Mchungaji tajiri kuliko wote Nigeria, Mchungaji David Oyedepo
Uchunguzi uliofanywa nchini Nigeria umebaini kuwa wachunga kondoo wa Bwana nchini humo mbali ya kuhubiri neno la bwana wanatengeneza pesa ya maana kiasi cha kwamba baadhi yao wanamiliki ndege, hoteli na biashara kubwa.Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Muandishi wa Nigeria wa jarida la Marekani la masuala ya uchumi, Forbes, wahubiri wa neno la bwana nchini Nigeria wanatengeneza pesa sana kutokana na uchungaji kiasi cha kufanananishwa na matajiri wa biashara ya mafuta.
Mfonobong Nsehe akitoa ripori ya uchunguzi wake alisema kuwa wachungaji wa Nigeria wanaishi maisha ya kifahari na wana miradi mikubwa ya kibiashara.
"Kuhubiri ni biashara inayolipa sana, sawa sawa na biashara ya mafuta", alisema Nsehe.
Utajiri wa wachungaji watano maarufu nchini Nigeria unakadiriwa kufikia dola milioni 200, alisema Nsehe.
Makanisa mengi yameibuka nchini Nigeria na waumini wamekuwa wakiongezeka.
Nsehe alisema kuwa mchungaji tajiri kuliko wote ni Mchungaji David Oyedepo wa kanisa la Living Faith World Outreach Ministry, ambaye utajiri wake ni dola milioni 150.
Mchungaji Oyedepo ndiye anayeshika nafasi ya pili akimiliki ndege nne, kampuni ya uchapishaji, chuo kikuu na shule moja na majumba ya kifahari jijini London na Marekani.
Mchungaji Chris Oyakhilome wa kanisa la Loveworld Ministries ana utajiri unaokadiriwa kuwa kati ya dola milioni 30 na 50. Mchugaji Oyakhilome anamiliki kampuni ya magazeti na majarida, stesheni ya televisheni, hoteli na kampuni ya majumba.
"Wachungaji hawa wanaishi maisha ya kifahari utawaona kwenye ndege zao binafsi na magari ya kifahari", alisema Nsehe.
Wachungaji wengine walioingia kwenye listi ya utajiri ni mchungaji Temitope Joshua Matthew mwenye utajiri kati ya dola milioni 10 na 15, Mchungaji Matthew Ashimolowo dola milioni 6-10, na mchungaji Chris Okotie mwenye utajiri kati ya dola milioni 3-10.
Nsehe aliongeza kuwa wawakilishi wa wachungaji wote isipokuwa mchungaji Ashimolowo, wamethibitisha taarifa ya umiliki wa mali za wachungaji hao.
Ukiwa Mchungaji Kanisani Nigeria, Utajiri Nje Nje
Mfanyabiashara maarufu Zanzibar atinga kizimbani
Mfanyabiashara maarufu mjini Zanzibar Suleyum Mbarak Salim (35) amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuiibia Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Sh bilioni 2.7.
Mfanyabiashara huyo, maarufu kama Morgan alisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu, Amisa Suleima Hemed wa Mahakama ya mkoa mjini Magharibi Unguja jana.
Mwendesha mashtaka wa serikali, Maullid Mkame alisema mshtakiwa huyo anadaiwa kuiibia benki ya watu wa Zanzibar kati ya Machi 12 na Mei 11, 2009.
Alisema kwamba mstakiwa aliiba dola za Marekani 122,000 sawa na sh bilioni 2.7, ikiwa ni mali ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kitendo ambacho ni kinyume na sheria namba 6 kifungu namba 124 (1) (4) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ya mwaka 2004. Mshtakiwa alikana shtaka hilo ambapo wakili anayemtetea Suleiman Salum aliomba mteja wake kupatiwa dhamana kwa vile shtaka alilofunguliwa ni miongoni mwa makosa yenye dhamana na haki yake kwa mujibu wa katiba.
Salum alisema kwamba mshtakiwa hajawahi kuhusishwa na mashtaka yoyote au kutiwa hatiani kwa kosa lolote na kuomba hakimu kumpatia dhamana mteja wake kwa vile ana mali zisizohamishika.
Hata hivyo, mwendesha mashtaka, Maulid Makame alisema kwamba kwa muda mrefu, mshtakiwa huyo alikuwa akisakwa baada ya kuhusishwa na kesi namba 115 inayohusu wizi katika benki hiyo ya Zanzibar iliyofunguiliwa mwaka 2009 na kuwahusisha wafanyakazi wawili wa benki hiyo.
Alisema kitendo cha kumpa dhamana kinaweza kuathiri upelelezi hasa kwa kuzingatia uchunguzi wa suala hilo haujakamilika na mshtakiwa alikuwa anasakwa muda mrefu.
Hata hivyo, Hakimu Amisa alisema atatoa uamuzi juu ya ombi la dhamana Juni 23, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena katika mahakama ya Vuga mjini Zanzibar.