Jela Maisha Kwa Kumpachika Mimba Binti wa Miaka 9
Fede DatilusSaturday, March 26, 2011 2:42 AM
Mwanaume mmoja wa nchini Marekani amehukumiwa kwenda jela maisha kwa kumpachika mimba mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 9.Fede Datilus wa Florida nchini Marekani amehukumiwa kwenda jela maisha kwa kumpachika mimba msichana mwenye umri wa miaka 9 raia wa Haiti.
Datilus lipatikana na hatia ya kumbaka msichana mwenye umri chini ya miaka 12 kosa ambalo aliadhibiwa kifungo cha maisha.
Datilus alipatikana na hatia ya kosa jingine la kumpachika mimba msichana mwenye umri wa miaka 9 kosa ambalo alihukumiwa kwenda jela miaka mitano.
Msichana aliyepachikwa mimba alikuwa ni raia wa Haiti amabye alihamia Marekani pamoja na wazazi wake miaka miwili iliyopita.
Baba wa msichana huyo aligundua mtoto wake ni mjamzito mwezi machi mwaka jana baada ya kumpeleka kliniki alipokuwa akiumwa.
Msichana huyo ambaye jina lake halikutajwa kwa sababu za kisheria alifanikiwa kumtambua Datilus kuwa ndiye mwanaume aliyembaka.
Msichana huyo alijifungua salama mwa huu akiwa amefikisha umri wa miaka 10.
Datilus mwenye umri wa miaka 33, alihukumiwa kwenda kuyamalizia maisha yake yaliyobakia jela.
Kelvin Etuhu
Mshambuliaji wa Manchester City, Kelvin Etuhu ametupwa jela miezi minane kwa kumpiga mtu mtaani na kumvunja taya.Mshambuliaji wa timu tajiri ya nchini Uingereza Manchester City, Kelvin Etuhu ametupwa jela miezi minane kwa kumpiga mtu mtaani na kumvunja taya lake.
Etuhu ambaye alisomewa mashtaka yake katika mahakama ya mjini Manchester alipatikana na hatia ya kufanya shambulizi la kudhuru mwili na kufanya vurugu.
Etuhu mweye umri wa miaka 22 baada ya kupata ulabu alimshambulia mwanaume mmoja aliyekuwa akizozana naye ndani ya baa mwaka jana, Etuhu alionekana kwenye CCTV akiendelea kumshushia kipigo mwanaume huyo baada ya kumtandika ngumi iliyomdondosha chini.
Etuhu ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Nigeria, amehukumiwa kwenda jela miezi minane.
source nifahamishe
Moshe KatsavWednesday, March 23, 2011 1:57 AM
Hatimaye Rais wa zamani wa Israel, Moshe Katsav ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya ubakaji, amehukumiwa leo kwenda kunyea debe jela kwa miaka saba.Aliyekuwa rais wa Israel Moshe Katsav amehukumiwa kwenda jela miaka saba kwa makosa ya ubakaji na makosa mengine ya kuwashambulia wanawake.
Wakitoa hukumu ya kesi hiyo iliyochukua miaka minne, majaji watatu wa kesi hiyo walimuadhibu rais huyo mkware kwa kumuweka kwenye kundi la watu ambao hawatapata msamaha wowote wa kutoka jela katika miaka miwili ijayo.
Katsav pia alihukumiwa kumlipa fidia ya dola 27,000 mwanamke aliyemfikisha mahakamani anayejulikana kwa jina la "Aleph".
Mwezi disemba mwaka jana Katsav alipatikana na hatia ya kubaka, kufanya shambulizi la kijinsia na kuizuia sheria kushika mkondo wake.
Wakati hukumu ikitolewa mmoja wa watoto wa rais huyo wa zamani wa Israel alimsogelea baba yake ili aweze kumkumbatia na baba yake alipiga kelele kwa sauti akisema "Usihofu Hawajatenda haki".
"Uongo umeushinda ukweli, Wanajua wameongopa", Katsav aliwaambia majaji wa kesi hiyo akiwaashiria wanawake waliomfikisha mahakamani kwa ubakaji.
Mmoja wa majaji alimwambia Katsav kuwa kosa la ubakaji linaharibu utu wa mtu na hivyo lazima adhabu iwe kali.
"Mtuhumiwa ametenda kosa kubwa na kama watu wengine ataadhibiwa, Hakuna mtu aliye juu ya sheria", alisema jaji huyo.
Mapenzi Yamzingua Bibi wa Miaka 92, Ampiga Mtu Risasi
Bibi Helen Staudinger
Bibi mwenye umri wa miaka 92 wa nchini Marekani ametiwa mbaroni kwa kumpiga risasi mwanaume jirani yake ambaye alikataa kumpa 'denda' bibi huyo ambaye alizidiwa na penzi kwa jirani yake ambaye siku zote alikuwa akimtolea nje bibi huyo.Bibi Helen Staudinger mjane mwenye umri wa miaka 92 mkazi wa Florida nchini Marekani ametiwa mbaroni kwa kuishambulia kwa risasi nyumba ya jirani yake ambaye alikataa kumpa busu.
Helen aliwaambia polisi kuwa alienda kwa jirani yake mwenye umri wa miaka 53, Dwight Bettner, na kumuomba ampe angalau busu ili autulize moyo wake uliojaa cheche za mapenzi kwa jirani huyo.
Baada ya Dwight kukataa kumbusu Helen, Helen alisema kuwa hataondoka mlangoni kwake hadi pale Dwight atakapokubali kumbusu.
Helen aliwaambia polisi kuwa mzozo mkubwa ulizuka kati yake na Dwight na kupelekea bibi huyo arudi nyumbani kwake kuchukua bunduki na kuanza kuishambulia kwa risasi nyumba ya Dwight.
Mojawapo ya risasi ilipenya kwenye dirisha la chumba cha Dwight na kusababisha Dwight kujeruhiwa na vioo va dirisha hilo. Risasi zingine tatu zilipigwa kwenye kuta za nyumba ya Dwight.
Dwight aliliambia gazeti la Star-Banner kuwa kwa miezi sita tangu alipohamia nyumba ya jirani na bibi Helen, amekuwa akisumbuliwa na bibi huyo anayemtaka kimapenzi.
"Nilimwambia kuwa nina uhusiano na mwanamke mwingine lakini alikuwa akisisitiza lazima niwe mpenzi wake", alisema Dwight.
Dwight aliongeza kuwa bibi Helen aliwahi kumshambulia mwanamke mmoja ambaye alifikiria alikuwa ndiye mpenzi wa Dwight.
Bibi Helen amefunguliwa mashtaka ya kufanya shambulizi la silaha kwenye makazi ya watu.
Sandra Torres de ColomMke wa rais wa Guatemala ameamua kuivunja ndoa yake ya miaka minane ili aweze kugombea urais. Mahakama ya nchini Guatemala imeanza kusikiliza kesi ya mke wa rais wa Guatemala ambaye ameenda mahakamani kudai talaka ili kuivunja ndoa yake ya miaka minane na rais Alvaro Colom.
Mke huyo wa rais, Sandra Torres de Colom ameamua kuivunja ndoa yake ili aweze kuwania kiti cha urais ambacho mume wake atakiachia atakapomaliza muda wake mwezi septemba mwaka huu. Mume wake anamaliza miongo yake miwili ya uongozi na hataruhusiwa kugombea tena urais.
Sheria za Guatemala zinakataza watu wa familia ya rais kushiriki kwenye uchaguzi wa kugombea urais.
Sandra alitangaza wiki iliyopita kuwa atagombea urais mwaka huu kwa kupitia chama tawala National Unity for Hope party.
Kama rais Colom atakubali kutoa talaka kuivunja ndoa yake basi Sandra ataruhusiwa kisheria kugombea urais.