Magari Saba Ya Kifahari Kwaajili ya Wake wa Rais

Sunday, March 06, 2011 / Posted by ishak / comments (0)

Pamoja na kwamba ana ndege yake maalumu ya kiraisi na msururu wa magari ya serikali anayoambatana nayo katika misafara yake, rais Jacob Zuma anatafuta magari saba ya kifahari kwaajili ya wake zake.
Kamati ya ulinzi wa rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma imetangaza kutoa tenda ya kukodisha magari saba ya kifahari kwaajili ya wake wa rais Zuma .

Katika miji saba ya Afrika Kusini ukiwemo mji anaotoka Jacob Zuma wa KwaZulu-Natal kutakuwepo na gari moja ambalo litakuwa tayari tayari kwaajili ya wake wa Rais Zuma.

Kwa mujibu wa nyaraka za tenda ya kukodisha magari hayo, magari yanayohitajika yanatakiwa yawe ni magari mapya ya kifahari na magari hayo lazima yawe ni aidha Mercedes-Benz S600, BMW 7 series, Audi A8 au A6, Mercedes-Benz ML, BMW X5 series, Audi Q7, Toyota Prado, Toyota Land Cruiser au Nissan Pathfinder.

Rais Zuma amewahi kuwaoa wanawake watano ambapo mwanamke mmoja kati yao, Nkosazana Dlamini-Zuma, alimpa talaka mwaka 1998 wakati mke wake mwingine toka Msumbiji, Kate Mantsho, alijiua mwenyewe mwaka 2000.

Hivi sasa Zuma anaishi na wake zake watatu Gertrude Sizakele, Nompumelelo Ntuli (MaNtuli) na Thobeka Stacie Madiba.

Zuma pia ana wachumba wawili ambao amepanga kuwaoa katika siku za karibuni.

nifahamishe source