Yanga Yaiua Simba Yatinga Fainali Tusker Cup

Friday, December 25, 2009 / Posted by ishak / comments (0)


YANGA imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Tusker baada ya kuifunga Simba mabao 2-1 kufuatia mchezo wa nusu fainali uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga ndio waliokianza kipindi cha kwanza kwa kasi na kusukuma mashambulizi langoni mwa Simba katika dakika ya kwanza tu ya mchezo nusura waandike bao baada ya mabeki wa Simba na kipa wao Juma Kaseja kujichanganya lakini Jerry Tegete akawa mziko kuuwahi mpira uliokuwa unazubaa.

Wanajangwani waliendelea kushambulia mfululizo lakini katika dakika ya tano, Simba walizinduka na Mussa Hassa Mgosi alipiga shuti kali lililokua linajaa wavuni lakini kipa Mghana wa Yanga, Yaw Berko aliliona na kupangua na kuwa kona tasa.

Dakika moja baadaye, Mrisho Ngassa aliambaa na mpira tokea katikati ya uwanja huku mabeki wa Simba wakishindwa kumthibiti na alifanikiwa kupiga krosi ‘ndizi’ ambayo hata hivyo beki Kelvin Yondani aliiwahi na kuitoa nje na kusababisha kona ambayo hata hivyo haikuzaa bao.

Kiungo mpya wa Simba, Jerry Santo nusura aipatie timu yake bao katika baada ya kuachia shuti kali pembeni mwa uwanja lakini mara nyingine, Berko alikuwa makini na kupangua mpira huo uliozaa kona.

Kwa ujumla katika kipindi cha kwanza, Yanga ndio waliotawala kipindi cha kwanza na kufanya mashambulizo mengi zaidi wakifanikiwa kutengeneza nafasi saba za kkufunga huku watani wao Simba wakitengeneza nafasi tatu tu.

Katika kipindi hicho Yanga ilipata kona tatu na watani wao Simba wakapata tatu lakini hakuna iliyozaa bao. Huku mwamuzi kutoka Uganda akiwazawadia kadi za njano wachezaji Amir Maftah, Ngassa (Yanga), Yondani na Emmauel Okwi (Simba).

Yanga ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 67 kupitia kwa Jerry Tegete baada ya pasi nzuri iliyopigwa na Abdi Kassim kuuvuka ukuta wa Simba uliokuwa ukijichanganya tangu mwanzo wa mechi.

Baada ya bao hilo Simba walionekana kuchanaganyikiwa na kuwapa nafasi Yanga kushambulia zaidi hata hivyo hawakuwa makini kumalizia.

Dakika ya 78 Okwi aliangusha ndani ya eneo ya eneo la hatari na Cannavaro na mwamuzi kuamuru penalti ipigwe na Hilary Echesa akafunga kwa ufundi huku kipa Obren Cuckovic aliyeingia katika kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Berko aliyeumia akishindwa kuzuia.

Mabao hayo yalidumu hadi dakika 90 na mwamuzi Dennis Batte wa Uganda kuamua kuongeza dakika ambapo katika dakika ya 120, Shamte Ally aliipatia Yanga bao la pili na laushindi baada ya kuitumia vema pasi ya Mrisho Ngassa.

Kwa matokeo hayo, Yanga itacheza na Sofapaka katika mchezo wa fainali keshokutwa Jumapili.

source.nifahamishe

Adakwa Live Akiwabaka Farasi

Friday, December 25, 2009 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanaume mmoja wa nchini Marekani ambaye alikodisha nyumba karibu na uwanja wa mashindano ya farasi ili aweze kupata nafasi ya kufanya mapenzi na farasi, amedakwa live akiwa juu ya farasi.
Kijana Erick Rivera mwenye umri wa miaka 18 anakabiliwa na mashtaka matano ya kuwafanyia ukatili wanyama baada ya kunaswa akifanya mapenzi na farasi.

Taarifa zilizotolewa na polisi zilisema kwamba Rivera alikodisha chumba karibu na uwanja wa mashindano ya farasi wa Hudson Valley uliopo Goshen, Indiana ili aweze kumalizia haja zake za kimapenzi kwa farasi waliokuwa wakihifadhiwa kwenye mazizi ya farasi yaliyopo kwenye uwanja huo.

Kuanzia mwezi julai mwaka huu uchunguzi wa polisi ulianza katika mazizi ya farasi hao baada ya watu wanaowatunza farasi hao kukuta stuli kwenye mazizi hayo.

Baada ya uchunguzi wa polisi wa miezi sita iligundulika kuwa Riviera alikuwa akiwanyatia farasi hao nyakati za usiku na kufanya nao mapenzi.

Polisi walifanikiwa kupata video za kamera za ulinzi zikimwonyesha Rivera akifanya kitendo hicho.

Rivera amefunguliwa makosa matano ya ukatili kwa wanyama na kufanya wizi.

Rivera ametupwa mahabusu akisubiri hukumu yake huku dhamana yake ikiwa ni dola 15,000.

source.nifahamishe

Faza Krismasi Safari Hii Hakutoa Zawadi, Apora Pesa

Friday, December 25, 2009 / Posted by ishak / comments (0)


Faza Krismasi huyu wa nchini Marekani hakuwa kama wenzake, hakuja kwa nia ya kutoa zawadi kama kawaida, yeye alivamia benki na kupora pesa.
Mwanaume mmoja wa nchini Marekani akiwa amevalia mavazi ya Faza Krismasi (Santa) aliiteka benki katika mji wa Nashville, Tennessee na kupora pesa na kisha kutoroka.

Faza Krismasi huyu ambaye tofauti na wenzake ambao hubeba zawadi, yeye alibeba bunduki na kuwatishia wahudumu wa benki ya SunTrust Bank wasalimishe pesa zote walizo nazo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na polisi, faza krimasi huyu wa bandia jana asubuhi aliingia kwenye benki hiyo akiwa na kiroba chekundu ambacho alikiweka juu ya meza ya mhudumu wa benki na kisha kutoa bunduki yake akiwaamuru watu wote waliokuwepo kwenye benki hiyo walale chini.

Baada ya kukijaza kiroba chake pesa, faza krismasi huyo alitoka taratibu na kupanda gari la rangi ya kijivu lililokuwa likimsubiria nje ya benki hiyo.

Wakati akiondoka zake, faza krimasi huyo aliwaambia watu waliokuwepo kwenye benki hiyo kuwa "Faza Krismasi anahitaji pesa za kuwalipa wasaidizi wake".

Kiasi cha pesa kilichoibwa toka katika benki hiyo hakijajulikana na polisi wameanzisha msako wa kumtafuta faza krimasi huyo feki.

source.nifahamishe.com

BREAKING NEWS - Mwanamke Ampiga Mwereka Papa Benedict Wakati wa Misa ya Krismasi

Friday, December 25, 2009 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanamke mmoja wa nchini Italia anashikiliwa na polisi baada ya kuruka vizuizi vya ulinzi na kumpiga mwereka Papa Benedict XVI wakati akielekea kufungua misa ya krismasi katika kanisa la St. Peter mjini Vatican.
Mwanamke aliyefanikiwa kuruka vizuizi vya ulinzi, alimpiga mwereka Papa Benedict XVI aliyekuwa akielekea mbele ya kanisa kuanzisha misa ya krismasi katika kanisa la St Peter mjini Vatican.

Katika tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia leo ijumaa, Mchungaji Ciro Benedettini aliyekuwa karibu na Papa alisema kuwa Papa aliamka kutoka chini mwenyewe baada ya kuangushwa na mwanamke huyo.

Papa mwenye umri wa miaka 82 hakupata jeraha lolote katika tukio hilo lakini alionekana kutetereka wakati walinzi na wasaidizi wake walipokuwa wakimuongoza kuelekea kwenye altare kuu kuiongoza misa ya krismasi.

Mchungaji Benedettini alisema kuwa mwanamke aliyemwangusha chini Papa alionekana kuwa na matatizo ya akili na alikamatwa na polisi wa Vatican.

Pia mwanamke huyo alimsukuma na kumwangusha chini kardinali Roger Etchegaray, ambaye alipelekwa hospitali kwa uchunguzi zaidi wa afya yake.

Baada ya tukio hilo Papa aliiongoza misa ya krismasi kama kawaida na hakugusia hata kidogo tukio la kuangushwa chini na mwanamke huyo.

Aliianzisha misa ya Krismasi kama ilivyo desturi kwa maneno ya kilatino ya kuwatakia watu amani kwa kusema "Pax vobis" ("Amani iwe juu yenu") na waumini walijibu "Et cum spiritu tuo" ("Iwe juu yako pia").

Hii ni mara ya pili kwa mwanamke kuruka viunzi vya ulinzi na kujaribu kumdondosha Papa. Wakati wa misa ya mwaka jana, mwanamke mmoja aliviruka vizuizi vya ulinzi na kumfikia Papa lakini kabla hajafanya chochote walinzi walimwahi na kumweka chini ya ulinzi.

Haijajulikana mara moja kama mwanamke aliyemdondosha Papa safari hii ndio yule yule wa mwaka jana au la.


source.nifahamishe

mtanzania aliyeuawa uingereza

Wednesday, December 23, 2009 / Posted by ishak / comments (0)Salum Kombo,mtanzania alieuawa nchini uingereza
href="http://3.bp.blogspot.com/__R2dXloMrWE/SzHzMBbD9LI/AAAAAAAAAQc/zfWEGGzetjE/s1600-h/1261554632_marafiki_wa_kombo.jpg">
marafiki zake wakimlilia kwa huzuni kubwa

sehemu ya tukio lilipotokea
SALUM KOMBO, kijana mwenye umri wa miaka 18, Mtanzania ambaye ameishi Uingereza kwa muda wa miaka ipatayo saba, jana ameshambuliwa kwa kisu na kufa kutokana na kilichoelezwa kuwa "mgogoro mdogo" uliotokana na mtandao (tovuti) unaotumiwa na watu, hususani marafiki au watu wenye uhusiano wa karibu, kuwasiliana juu ya mambo mbalimbali uitwao Facebook...

Uzio wa Hoteli ya kitalii wabomolewa ni siku tatu toka izinduliwe na R

Wednesday, December 23, 2009 / Posted by ishak / comments (0)


UZIO WA HOTELI ya kitalii iitwayo Snow Crest ya jijini Arusha, imebomolewa uzio uliozunguka hoteli hiyo na kuharibu miundombinu mizima ya mawasiliano hotelini hapo baada ya kudaiwa kuwa umejengwa kwenye eneo la hifadhi.
Ukuta huo ulibomolewa jana majira ya saa 11:30 za asubuhi, na Wakala wa barabara nchini [TANROADS] kwa kudai uzio huo umejengwa kimakosa na umezidi eneo la hifadhi ya taifa.

Hatua hiyo ya Tanroads imekuja ni baada ya siku tatu toka Rais wa nchi, Jakaya Kikwete kwenda kuzindua hoteli hiyo ya kitalii mjini humo Ijumaa wa wiki iliyopita.

Meneja wa Hoteli hiyo Bw. Mark Digira aliwaambia vyombo vya habari kuwa Kutokana na kuvunjwa kwa ukuta huo imeharibu hadhi ya hoteli hiyo ambayo I imejengwa kwa mabilioni ya fedha.

Na kusema kuwa labda kuna hujuma maana kama kungekuwa na kasoro hizo wakala wa barabara wangezuia toka hoteli hiyo inajengwa lakini amewsema wao hawakupata kibali chochote kutoka kwenye taasisi hiuyo iliyoashiria wasijenge eneo hilo na ingekuwa hivyo wasingeweza kufanyia hivyo.

Amesema hoteli hiyo iligharamia kiasi cha shilingi bilioni 8 za kitanzania kujenga hoteli hiyo ya kitalii iliyozinduliwa na Rais Kikwete.

Wakizungumza na vyombo vya habari ene o la tukio, wakala hao wa barabara walisema sababu iliyofanya ibomoe uzio huo ni Kutokana kujengwa na kuchota mita 22 na nusu ya hifadhi ya taifa.

Wamesema hiyo ndiyo sababu kubwa iliyofanya uzio huo ubomolewe kwa kuwa walimega eno hilo ambalo haliwahusu kwen yeujenzi huo wa hoteli.
Hoteli hiyo ya Snow Crest ipo mijini Arusha kwenye barabara iendayo Moshi Arusha.

HAta hivyo wadau mbalimbali wakiwemo na wakazi wa mjini humo kitendo cha Tanroads kimechukuliwa ni sawa na kumdharau rais Kikwete aliyekwenda kuzindua hoteli hiyo.

source.nifahamishe.com

Mtoto Yatima wa Miaka 10 Amuua Mama Aliyejitolea Kumlea

Wednesday, December 23, 2009 / Posted by ishak / comments (0)


Mtoto mwenye umri wa miaka 10 wa nchini Thailand ambaye alinusurika kufariki wakati wa tufani la Tsunami nchini humo lililowaua wazazi wake wote wawili, amefunguliwa mashtaka ya mauaji ya mwanamke aliyejitolea kumlea ambaye alikuwa akimbeza kuhusiana
Polisi wa Jakarta Indonesia walimfungulia mashtaka mtoto huyo baada ya kumkuta mwanamke aliyejitolea kumlea Etty Rochyati mwenye umri wa miaka 55, akiwa amefariki baada ya kupigwa na kitu kizito na kuchomwa chomwa na kisu tumboni, limeripoti gazeti la Jakarta Globe .

Maiti ya mwanamke huyo ilikutwa kwenye kiambaza cha nyumba yake akiwa na majeraha mengi kichwani na majeraha ya kisu tumboni mwake.

Mtoto huyo ambaye jina lake halikutajwa kwa sababu ya umri wake mdogo, aliwaambia polisi kuwa mwanamke huyo alikuwa akimnyanyasa kwa maneno akimwambia “Hujui kuwa wewe huna baba wala mama?” na wakati mwingine alikuwa akitishia kumfukuza nyumbani kwake asipofuata amri zake.

Mtoto huyo alinusurika kwenye gharika la Tsunami lililokiteketeza kijiji chake kwenye kisiwa cha Nias ambapo wazazi wake wote wawili walifariki.

Mtoto huyo anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela iwapo atapatikana na hatia lakini taasisi ya kutetea haki za watoto nchini humo inapigania mahakama imhukumu mtoto huyo kama mtoto na hivyo kutoa adhabu ndogo.

“Kitu alichokifanya mtoto huyu kinaweza kuhesabika kama kitendo cha kujilinda kutokana na manyanyaso na wala hakukusudia kufanya kitendo hiki”, alisema katibu wa taasisi hiyo Arist Merderka Sirait.

“Hapa hatudili na kesi ya mwanaume wa miaka 22, tuna mtoto wa miaka 10 ambaye hajui chochote na ambaye ana maisha marefu baadae”, aliongeza katibu huyo.

Katibu huyo alisema kuwa familia ya mwanamke aliyeuliwa imekubaliana kuifuta kesi dhidi ya mtoto huyo na wapo katika taratibu za kuwasiliana na maafisa wa upelelezi na wanasheria kujua mustakbali wa kesi hiyo.


source.nifahamishe.com

Mfanyabiashara wa Kihindi Akamatwa na Kilo 8 za Almasi

Wednesday, December 23, 2009 / Posted by ishak / comments (0)


Mfanyabiashara mmoja toka India amekamatwa nchini Jamhuri ya Kongo akiwa na begi lililojaa zaidi ya kilo nane za madini ya almasi yasiyosafishwa akijaribu kuyasafirisha madini hayo kinyemela toka nchini humo.
Mfanyabiashara huyo aliyetajwa kwa jina la Ajudiya Pravin Kumar amehukumiwa kwenda jela miezi sita pamoja na kulipa faini ya dola laki moja za Kimarekani.

Kumar ambaye ni mfanyabiashara wa madini ya almasi alikuwa akiendesha biashara zake nchini humo kwa zaidi ya miaka sita.

Kumar alikuwa akitafutwa na mahakama kuu ya Gombe, Kinshansa akituhumiwa kusafirisha kiholela, kumiliki isivyo halali madini ya almasi na kujaribu kuwahonga maafisa wa Jamhuri ya Kongo.

Awali mwendesha mashtaka wa serikali alitaka Kumar ahukumiwe kwenda jela miaka 17 pamoja kulipa faini ya dola milioni 500 kwa hasara ambayo ameisababishia serikali ya Kongo.

Lakini hakimu wa kesi hiyo aliamua Kumar atumikie kifungo cha miezi sita jela pamoja na kulipa faini ya dola 100,000 huku madini hayo ya almasi yakitaifishwa kwa serikali.

Madini hayo yalipofanyiwa utafiti na wataalamu wa madini wa Jamhuri ya Kongo, yaligundulika kuwa na uzito wa karati 42,000 na yakiwa na thamani ya dola 500,000.

Wakili wa serikali alipinga hukumu iliyotolewa akisema haitoi funzo kwa wafanyabiashara wengine wanaouza almasi kimagendo na aliongeza kuwa anasubiria waziri wa sheria atoe malalamiko yake kwa hukumu hiyo.

Kumar alikamatwa tarehe 10 mwezi huu kwenye uwanja wa ndege wa Kinshansa akijaribu kuyasafirisha madini hayo aliyoyaficha kwenye begi lake akiyapeleka India.

Wakati wa taratibu za ulinzi uwanjani hapo, polisi mwanamke wa uwanja wa ndege alikuta mfuko wa Rambo ndani ya begi la Kumar ukiwa na madini ya almasi ambayo yalikuwa hayana hati husika za kuyasafirisha nje ya nchi hiyo.

Katika utetezi wake Kumar alijitetea kuwa alikuwa hana nia ya kusafirisha madini ya almasi akiendelea kusema kuwa alikuwa hajui kuwa amenunua almasi yeye alijua amenunua vito kwa ajili ya kutengenezea shanga na vidani vya wanawake.

source.nifahamishe.com

Miujiza ya Kijana Aliyefariki Yawapagawisha Wengi

Wednesday, December 23, 2009 / Posted by ishak / comments (0)


Mamia ya watu wanamiminika kwenye nyumba ya kijana mmoja nchini Australia ambaye muda mfupi baada ya kufariki kuta za nyumba yake zimeanza kutoa mafuta ya ajabu ambayo yanadaiwa kuwatibu watu magonjwa yao.
Wazazi wa kijana Mike Tannous aliyefariki miaka mitatu iliyopita wanadai kuwa kijana wao amechaguliwa na mungu kuwa mtawa wa kwanza wa kiume wa Australia.

Mike alifariki mwezi septemba mwaka 2006 akiwa na umri wa miaka 17 kutokana na ajali ya gari lakini wiki chache baadae kuta za chumba chake zilianza kutoa mafuta ya ajabu ambayo yanadaiwa kuwatibu mamia ya watu magonjwa yao.

Wazazi wake Mike, George na Lina wanaoishi katika kitongoji cha Guildford katika jiji la Sydney wamedai kuwa kijana wao ni mjumbe wa mungu na ameishawatibu watu wengi sana kwa miujiza yake.

Mafuta yanayomiminika kwenye kuta za nyumba yake yamefanyiwa uchunguzi wa kisayansi na wataalamu mbali mbali lakini bado hayajagundulika ni mafuta ya aina gani.

Mamia ya watu wamekuwa wakimiminika kwenye nyumba yao kuyaona na kusali wakiomba yawatibu magonjwa yao.
“Mtoto wetu ni mtawa, anazungumza nasi na anazungumza na watu kwa njia hii”, alisema baba wa kijana huyo.

“Mwaka jana mwanamke mmoja anayeishi karibu na nyumba yetu aliambiwa na madaktari hataweza kupata mtoto wa tatu kwa njia yoyote ile, alikuja hapa na kuanza kusali… mwezi mmoja baadae alirudi na boksi la biskuti akitamba kuwa amepata ujauzito”, alisema shangazi yake Mike, Susan Sawan.

Mamia ya watu wamekuwa wakimiminika kila siku kwenye nyumba hiyo na hivi sasa si kuta za chumba chake pekee zinazovuja mafuta bali kuta zote za nyumba hiyo ya vyumba vitatu mpaka kwenye picha ya Mike ukutani.

“Mwishoni mwa wiki watu huja toka sehemu mbali mbali na kutufanya tufunge mtaa, wanataka kushuhudia miujiza”, alisema baba wa kijana huyo aliyefariki.

Kutokana na habari za miujiza ya tiba ya mafuta ya kuta za nyumba hiyo kusambaa, mamia ya watu kutokana nchi mbali mbali duniani nao wamekuwa wakimiminika Austalia kushuhudia mafuta hayo.

Wazazi wa Mike wamesema kuwa wao hawakusanyi mchango wowote toka kwa watu wanaofika kwenye nyumba yao wanachopenda wao ni kuona watu wakipatiwa tiba kutokana na miujiza ya mtoto wao.

Familia hiyo imekuwa ikiwajibu watu wasioamini wanaotilishia shaka miujiza ya mafuta hayo kwa kuwaambia “Njoo na ushuhudie mwenyewe”.

source.nifamishe.com

Wanafunzi Wanyonyana Sehemu za Siri Darasani

Wednesday, December 23, 2009 / Posted by ishak / comments (0)


Wanafunzi wawili wa shule moja ya msingi ya nchini Marekani wamesimamishwa masomo kwa kipindi kisichojulikana baada ya kunyonyana sehemu za siri darasani mbele ya wanafunzi wenzao huku mwalimu ambaye alikuwa darasani wakati huo akishuhudia naye amenyang’anywa leseni yake ya ualimu.
Wanafunzi hao wa darasa la nane katika shule moja ya msingi katika mji wa Houston, Texas nchini Marekani wamesimamishwa shule kwa kipindi kisichojulikana baada ya kupatikana na hatia ya kufanya kitendo nje ya maadili ya kishule.

Wanafunzi hao walinyonyana sehemu za siri mbele ya kundi la wanafunzi wenzao huku mwalimu mmoja akiwa ndani ya darasa hilo hilo akiendelea kuwaelekeza masomo wanafunzi wengine.

Taarifa zilizotolewa zilisema kwamba baadhi ya wanafunzi walitengeneza duara kumziba mwalimu wao asione kinachoendelea wakati wanafunzi hao wa shule ya msingi wakinyonyana sehemu za siri huku wanafunzi wengi wakishuhudia kitendo hicho.

Baada ya tukio hilo, mmoja wa wanafunzi alipeleka taarifa kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo ambaye alipeleka taarifa polisi.

Wanafunzi hao walikamatwa na kuwekwa mahabusu katika jela za watoto na walifunguliwa mashtaka mahakamani ya kuharibu utulivu darasani na kufanya kitendo kinyume na maadili mbele ya watu.

Wanafunzi hao ambao majina yao hayakutajwa kutokana na sababu za kisheria, walikiri makosa yao katika mahakama ya watoto ya Houston.

Mwanafunzi wa kike alikabidhiwa kwa wazazi wake wakati uchunguzi wa suala hilo ukiendelea huku mwanafunzi wa kiume akiendelea kushikiliwa na polisi.

Mwalimu aliyekuwa darasani wakati huo ambaye alishindwa kuzuia wanafunzi hao wasiendelee kufanya kitendo hicho, amenyang’anywa leseni yake ya ualimu.

source.nifahamishe.com

Mtanzania Auliwa Kwa Kuchomwa Kisu Uingereza

Wednesday, December 23, 2009 / Posted by ishak / comments (0)


Kijana wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 18 aliyekuwa akiishi na kusoma nchini Uingereza ameuliwa kwa kuchomwa kisu na kijana wa Kiingereza mwenye umri wa miaka 15 aliyekasirishwa na maoni mabaya aliyoyatoa kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Kijana wa Kitanzania Salum Kombo aliyekuwa akiishi na kusoma nchini Uingereza ameuliwa na rafiki yake wa karibu kijana wa Kiingereza mwenye umri wa miaka 15 aliyekasirishwa na maoni ambayo Salum aliyaandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Salum aliuliwa kwa kuchomwa na kisu shingoni na begani kwenye uwanja wa basketball uliopo karibu na nyumbani kwao.

Taarifa zilizopatikana zilisema kwamba rafiki huyo wa Salum aliandika maoni kwenye ukurasa wake wa Facebook akionyesha hasira zake kwa kutoalikwa katika party iliyoandaliwa na rafiki zake.

Salum alijibu maoni hayo kwa kuandika maoni ya kumkashifu rafiki yake huyo ambaye kutokana na kukasirishwa kwake alitishia kumuua lakini hakuna mtu aliyetilia maanani vitisho hivyo.

Salum ambaye alikuwa akisomea Sanaa kwenye chuo cha Tower Hamlets College jijini London alikutana na rafiki yake huyo kwenye uwanja wa basketball uliopo karibu na nyumbani kwao ambapo bila kutarajia rafiki yake huyo alimshambulia kwa kumchoma na kisu mabegani na shingoni.

Katika tukio lililotokea siku ya jumapili jioni mbele ya marafiki zake, Salum alijaribu kujikongoja kuelekea kwao huku damu kibao zikimtiririka lakini hakufika mbali na alifariki dakika chache baadae wakati akipewa huduma ya kwanza kwenye eneo la tukio hilo.

Muuaji wake amekamatwa na alipandishwa kizimbani jana jijini London.

Salum aliwasili Uingereza miaka saba iliyopita na alikuwa akiishi na shangazi yake jijini London.

Salum amekuwa kijana wa 13 ndani ya mwaka huu kuuliwa kutokana na mashambulizi ya visu jijini London.

source.nifahamishe.com
om