Mwizi wa nchini Japan ambaye kutokana na kufanya wizi kwa mwaka alikuwa akijiingizia kiasi cha pesa sawa na Tsh. Milioni 540 ametoa kitabu cha kuelezea jinsi ya kuiba kwenye majumba ya watu bila kugundulika, kitabu hicho kimekuwa gumzo nchini Japan na kinanuliwa kwa wingi.
Mwizi wa nchini Japan, Hajime Karasuyama kutokana na utaalamu wake wa kuiba kwenye majumba ya watu, ametoa kitabu kinachoelezea jinsi ya kuiba kwa ustadi mkubwa bila ya kugundulika.
Kitabu chake kinachoenda kwa jina la "Kazi: Mwizi, Kipato Kwa mwaka: Yen Milioni 30", kimekuwa gumzo nchini Japan na kimekuwa kikinunuliwa kama njugu.
Wachapishaji wa kitabu hicho Futabasha Publishing wamesema kuwa nakala za mwanzo za kitabu hicho zipatazo 10,000 zimenunuliwa zote ndani ya siku 10 baada ya kitabu hicho kuzinduliwa.
Katika kitabu hicho, Karasuyama anaelezea jinsi ya kufungua vitasa vya milango ya aina yoyote ile kwa muda mfupi na bila ya ufunguo na jinsi ya kuvunja madirisha ya vioo bila ya kusababisha kelele.
Karasuyama ameelezea pia jinsi alivyokuwa akitumia lensi kuangalia ndani ya nyumba kwa kupitia kwenye tundu la funguo.
Mbali ya wizi wa majumbani, Karasuyama pia amelezea pia njia za kufanya utapeli na kuwaacha watu kwenye mataa.
Karasuyama alisema kuwa kutokana na wizi alikuwa akijiingizia kitita kinono kwa mwaka zaidi ya Tsh. Milioni 540.
"Tunapoingia ndani ya nyumba, sisi wezi huwa tunajua wapi watu huficha pesa zao", alisema Karasuyama alipokuwa akiongea na jarida la Shukan Taishu kuhusiana na kitabu chake ambacho kimeambatanisha maneno ya "Usijaribu kuniiga" kwenye ukurasa wake wa kwanza.
Wachapishaji wa kitabu hicho kinachouzwa Yen 1,200 sawa na Tsh. 20,000 wamekanusha madai kuwa kuchapishwa kwa kitabu hicho kutapelekea baadhi ya watu kugeuka wezi kwa kuiga staili za wizi za Karasuyama.
Wachapishaji hao wamesema kuwa kitabu cha Karasuyama kitawawezesha watu kujifunza njia zinazotumiwa na wezi hivyo kuweza kuzilinda vyema nyumba zao.
source nifahamishe
Pamoja na serikali ya Marekani kuionya tovuti maarufu ya kutoboa siri zilizoficha ya WikiLeaks kutoziweka nyaraka zake za siri hadharani kwa kuwa maisha ya watu wengi yatakuwa hatarini, tovuti hiyo imezitoa nyaraka hizo za siri na kuiweka hadharani sura halisi ya Marekani.
Nyaraka za siri za Marekani zipatazo 250,000 zimeanza kuwekwa hadharani pamoja na serikali ya Marekani kuionya tovuti ya WikiLeaks kuwa inavunja sheria na inayaweka maisha ya watu wengi hatarini.
Tovuti ya WikiLeaks ambayo imebobea kwa kutoboa siri za ndani za masuala mbalimbali duniani ilikabiliwa na mashambulizi ya hackers ambao waliifanya tovuti hiyo ishindwe kupatikana online.
Hata hivyo nyaraka hizo za siri zimewekwa hadharani kama ilivyopangwa kwa kutumia magazeti ya The Guardian la Uingereza, gazeti la New York Times la Marekani, Der Spiegel la Ujerumani, El Pais la Hispania na gazeti la Le Monde la Ufaransa.
Nyaraka hizo za siri huenda zikaharibu uhusiano wa Marekani na baadhi ya viongozi wa nchi mbalimbali duniani ambao Marekani iliwapachika majina mbalimbali ya kuwakashifu.
Miongoni mwa nyaraka hizo za siri hizo ni mazungumzo ya siri kati ya Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia ambaye mara nyingi sana alikuwa akiishinikiza Marekani ipigane vita na Iran ili kuziteketeza silaha zake za nyuklia.
Taarifa hizo ziliendelea kusema kuwa Mfalme huyo wa Saudia aliishinikiza Marekani iiwekee Iran vikwazo vikali vya kiuchumi na kuwapiga marufuku viongozi wake kusafiri kimataifa.
Nyaraka hizo ziliendelea kusema kuwa Mfalme Abdullah aliungwa mkono na Mfalme wa Bahrain, Hamad ibn Isa Al Khalifa na Mtawala wa Abu Dhabi, Sheikh Mohammad bin Zayed ambao nao waliitaka Marekani iiteketeze Iran.
WikiLeaks pia ilitoa nyaraka ambazo zilisema kuwa Marekani kwa kuwatumia maafisa wake kinyume cha sheria iliwapeleleza viongozi wa baraza la Umoja wa Mataifa na hata kufikia kuchukua kwa siri alama za mboni ya jicho na alama za vidole za katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.
Marekani pia ilifuatilia simu walizokuwa wakipiga, fax, email na tovuti walizokuwa wakizitembelea.
Miongoni mwa majina ya kashfa waliyopachikwa viongozi wa serikali mbalimbali duniani, Marekani ilimuita Rais Mugabe wa Zimbabwe kuwa ni "Kichaa Mzee", kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi ameitwa "Mtu wa Ajabu Asiyeeleweka", wakati rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad amefananishwa na Hitler.
Nyaraka nyinginezo zilielezea jinsi Marekani ilivyokuwa ikizishinikiza baadhi ya nchi ziwachukue wafungwa wa kigaidi wa jela ya Guantanamo Bay. Nchi ya Slovenia ililazimishwa imchukue mfungwa mmoja wa Guantanamo Bay iwapo inataka kukutana na Rais Obama.
Nyaraka zaidi za siri zinazoonyesha jinsi Marekani ilivyokuwa ikivunja sheria za kimataifa zinaendelea kuchapishwa.
siurce nifahamishe
Rais wa Marekani, Barack Obama ameshonwa nyuzi 12 kwenye mdomo wake baada ya kupigwa kiwiko kwenye mdomo wake wakati akicheza mpira wa kikapu pamoja na ndugu na jamaa zake wa karibu.
Obama alikuwa akicheza mpira wa kikapu pamoja na ndugu na jamaa kwenye kambi ya jeshi la Marekani ya Fort McNair mjini Washington, wakati kwa bahati mbaya mcheza wa timu pinzani aliporusha kiwiko chake na kumtandika Obama mdomoni.
Msemaji wa ikulu ya Marekani alisema kuwa Obama alipasuka mdomo na alipatiwa matibabu na madaktari wa ikulu.
Hata hivyo taarifa ya ikulu ya Marekani haikusema ni nani ndiye aliyempasua Obama mdomo wake kwa kiwiko.
source nifahamishe