Siri ya Kimada Yafichuka

Friday, September 03, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mmoja wa wachimba madini wa nchini Chile ambao wamenasa mita 700 chini ya ardhi baada ya mgodi wa dhahabu waliokuwemo kuporomoka, ana kesi kubwa ya kujibu nyumbani akifanikiwa kutoka salama kwenye migodi hiyo baada ya mkewe kukutana na kimada wake kw
Mchimba madini wa nchini Chile ambaye amenasa mita 700 chini ya ardhi pamoja na wenzake 32, ana kesi kubwa ya kujibu akitoka salama kwenye migodi hiyo baada ya mkewe kukutana na kimada wake kwenye migodi hiyo.

Taarifa zilisema kuwa mke wa mchimba madini Yonni Barrios alihuzunika baada ya kugundua kuwa mumewe ana kimada na kimada huyo amekuwa akijitangaza kama jamaa wa karibu wa Barrios.

Mke wa Barrios anayeitwa Marta Silanas alisema kuwa alishtushwa sana baada ya kumsikia kimada wa mume wake, Susana Valenzuela akiliita jina la mumewe kwa sauti.

"Barrios ni mume wangu, ananipenda na mimi ni mke wake wa ndoa, huyu mwanamke hatambuliki kisheria", alisikika akisema Marta.

Lakini Susana naye hakukaa kimya, alijibu kuwa alikutana na Barrios miaka mitano iliyopita na wana mpango wa kufunga ndoa baada ya Barrios kuahidi atampa talaka mkewe ili wawe pamoja.

Susana alisisitiza kuwa ataendelea kumsubiria Barrios amuache mkewe.

Barrios na wenzake wamenasa mita 700 chini ya ardhi baada ya mgodi waliokuwemo kuporomoka, wataendelea kukaa huko chini kwa miezi minne zaidi wakati jitihada za kuwaokoa zitakapokamilika.

Kwa sasa wanatumiwa chakula, maji na madawa kupitia mashimo matatu madogo yaliyochimbwa ili kuwapitishia vitu hivyo kwa kupitia kwenye mabomba.

Barrios ni mtu muhimu sana miongoni mwa wachimba madini hao kwani yeye ndiye amekuwa akiwatibu wenzake kutokana na mafunzo ya huduma ya kwanza aliyochukua zamani.

source nifahamishe

Ajinyonga Baada ya Kunyimwa Mkopo

Friday, September 03, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanaume mmoja wa nchini Uturuki amejinyonga kwenye mlango wa kuingia kwenye sehemu aliyokuwa akifanya kazi baada ya kunyimwa mkopo na kampuni yake.
Mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Isa Uguten mwenye umri wa miaka 45, alijinyonga kwenye mlango wa kuingia kwenye uwanja wa klabu ya farasi ya mjini Adana ambako alikuwa akifanya kazi kama mtunza bustani.

Taarifa iliyotolewa ilisema kuwa kutokana na matatizo ya kifedha yaliyokuwa yakimkabili, Isa aliamua kuomba mkopo wa fedha toka kwa kampuni yake ambayo amekuwa akiifanyia kazi kwa miaka 15 sasa.

Hata hivyo kampuni yake ilikataa kumkopesha.

Baada ya kuambiwa hivyo, juzi usiku, Isa aliamua kujinyonga kwenye mlango wa kuingia kwenye viwanja vya klabu hiyo.

Mwili wake uligundulika jana asubuhi ukiwa unaning'ia kwenye mlango.

Polisi waliushusha chini mwili wake na aliposachiwa ilikutwa barua kwenye mfuko wake wa suruali akielezea sababu ya kujinyonga huku akiushushia lawama uongozi wa klabu hiyo.

Mwili wa Isa ulikabidhiwa kwa ndugu zake baada ya kukamilika kwa taratibu za uchunguzi wa maiti.

source nifahamishe

Mwanaume Anayemchezea Simba Sharubu

Friday, September 03, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Wakati watu wengi duniani hufuga mbwa na paka kwenye majumba yao, jamaa huyu wa nchini Iran yeye ameamua kufanya kitu cha hatari zaidi kwa kumfuga simba na kutembea nae mtaani.
Video ya mwanaume huyo akimuogesha simba kwa kutumia bomba la maji imekuwa maarufu kwenye mitandao mbalimbali duniani.

Katika VIDEO hiyo mwanaume huyo anaonekana akimshikilia simba pembeni ya barabara moja mjini Tehran na kumuogesha kama ambavyo watu huwaogesha mbwa wao.

Mamia ya watu wanaonekana wakiwa wamesimama pembeni wakimuangalia na wengine wakimpiga picha mwanaume huyo akimuogesha simba wake.


source nifahamishe

Urefu Wasababisha Aache Shule ya Msingi

Friday, September 03, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Msichana mwenye umri wa miaka 14 wa nchini Brazili ambaye ana urefu wa sentimita 206 amelazimika kuacha shule kwasababu amechoka kujipinda kwenye mabasi wakati wa kwenda shule, ameamua kuingia kwenye fasheni za mavazi.
Elisany Silva pamoja na kuwa na umri mdogo, ana urefu wa sentimita 206 na bado anaendelea kukua.

Elisany ameacha shule ya msingi na sasa anajiandaa kushiriki kwenye shoo yake ya kwanza ya fasheni za mavazi.

Kutokana na urefu wake Elisany anasema kuwa amechoka kujipinda kwenye mabasi wakati wa kwenda shule na pia anashindwa kucheza na watoto wenzake ambao amewazidi urefu zaidi ya nusu mita.

Urefu wake unasababishwa na maradhi ambayo hayajajulikana hata hivyo wazazi wake ambao ni masikini na hawana pesa za kulipia gharama za uchunguzi wa maradhi yake au kumpatia tiba, hawana mpango wa kujua ugonjwa alio nao.

"Nashindwa kufanya shughuli kama watoto wenzangu, nataka nicheze na marafiki zangu lakini siwezi", alisema Elisany.

"Napata shida ninapokuwa ndani ya nyumba yetu, nalazimika kujipinda ninapopita milangoni na mara nyingi sana najigonga kwenye paa la nyumba", aliendelea kusema Elisany.

Pamoja na matatizo ya familia yake, Elisany anatarajiwa kuwa nyota wa dunia wa baadae kwenye fasheni za mavazi kwani anarajiwa kuwa mwanamitindo mrefu kuliko wote duniani akivunja rekodi inayoshikiliwa na mrembo wa California, Marekani, Amazon Eve ambaye ana urefu wa sentimeta 205.

Elisany anatarajiwa kushiriki kwenye shoo yake ya kwanza ya mavazi katika mji wa Belem nchini Brazili ambapo atavaa shela za harusi.

source nifahamishe

Miaka 9 Jela Kwa Kuendesha Gari Huku Akiangalia Ngono

Friday, September 03, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Dereva wa lori wa nchini Marekani ambaye alikuwa akiendesha lori lake huku akiangalia video za ngono kwenye laptop na kupelekea ajali iliyosababisha kifo cha mtu mmoja amehukumiwa kwenda jela miaka 9.
Thomas Wallace wa Ohio nchini Marekani amehukumiwa kwenda jela miaka tisa baada ya kusababisha ajali iliyoua mtu mmoja.

Wallace alikuwa akiendesha lori lake huku akiangalia video za ngono kwenye laptop yake hali iliyopekea kuligonga gari la mlemavu na kupelekea kifo chake.

Mahakama iliambiwa kuwa siku ya tukio hilo disemba 12 mwaka jana, Wallace aliligonga gari la Julie Stratton, mwenye umri wa miaka 33 ambaye ni mama wa watoto wawili.

Akiongea mahakamani huku akimwaga chozi, Wallace mwenye umri wa miaka 45, aliiomba radhi familia ya marehemu kwa kusababisha ajali hiyo iliyopelekea wapoteze kipenzi chao.

Wallace alihukumiwa kwenda jela miaka 9 ingawa awali ilikisiwa angetupwa jela kati ya miaka mitano na 15.

source nifahamishe

Nywele Zilizokatiwa Bima ya Dola Milioni 1

Friday, September 03, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mchezaji mashuhuri wa soka la Kimarekani ambaye alijipatia maarufu kwa nywele zake ndefu, amezikatia bima ya dola milioni 1 nywele zake hizo.
Troy Polamalu mwenye umri wa miaka 29 ataendelea kutesa na nywele zake ndefu baada ya kampuni inayotengeneza shampoo za Head and Shoulder ya Procter & Gamble kuamua kuzikatia bima ya dola milioni 1 nywele zake hizo.

Iwapo Troy atakumbana na tukio lolote litakalopelekea apoteze nywele zake, kampuni ya bima italipa fidia zote.

Troy ambaye huichezea timu ya Pittsburg Steelers katika ligi ya NFL ya nchini Marekani ana nywele ndefu sana ambazo zina urefu wa mita moja.

source nifahamishe

Troy mbali ya nywele zake hizo, amejipatia umaarufu mkubwa kwa uchezaji wake wa soka la Kimarekani na amewahi kuchaguliwa kwenye NFL All Star kwa miaka mitano mfululizo.

Hata hivyo nywele zake hizo ambazo amedai amekuwa akizitunza kwa miaka 10 sasa, zimekuwa zikimsababishia matatizo uwanjani kwani baadhi ya wachezaji wa timu pinzani wamekuwa wakizitumia kuzivuta ili kumdondosha chini.

Madaktari Watupiana Makonde Chumba cha Uzazi

Tuesday, August 31, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mama mmoja wa nchini Italia pamoja na mtoto wake mchanga wanapigania maisha yao ambayo yameingia hatarini kufuatia ugomvi mkubwa uliozuka kwenye wadi ya uzazi baina ya madaktari wawili ambao walitakiwa kumzalisha mwanamke huyo.
Ugomvi mkubwa ulioisha kwa madaktari kujeruhiana na kutoana ngeu umepelekea maisha ya mama mmoja wa nchini Italia na mtoto wake mchanga yaingie hatarini.

Laura Salpietro, 30, alipoteza damu nyingi sana wakati wa uzazi na mtoto wake mchanga wa kiume aliyepewa jina la Antonio, alikumbwa na shambulio la moyo mara mbili kwenye wadi ya uzazi katika hospitali iliyopo Messina, Sicily.

Ugomvi mkubwa wa madaktari huo ulianza wakati bi Laura alipowasili hospitali akiwa amezidiwa na uchungu na hali yake ikiwa mbaya sana, madaktari katika hospitali hiyo walianza kubishana watumie njia ya asili au njia ya operesheni kumzalisha bi Laura.

Mabishano hayo kati ya dokta Vincenzo Benedetto na daktari wa wadi ya uzazi Antonio De Vivo yaligeuka kuwa ugomvi na madaktari hao walianza kurushiana makonde ya nguvu ndani ya wadi hiyo.

Mume wa bi Laura, Matteo Molonia alisema kuwa aliwasihi madaktari waache kupigana na wamsaidie mkewe ambaye hali yake ilizidi kuwa mbaya lakini madaktari hao hawakumsikiliza.

"Nipo kwenye hatihati ya kupoteza familia yangu kwasababu madaktari wameamua kupigana ndani ya wadi ya uzazi", alisema Molonia.

Hatimaye bi Laura alijifungua kwa njia ya operesheni lakini kutokana na kucheleweshwa kujifungua, maisha yake na ya mtoto wake yameingia hatarini.

Madaktari wote wawili wamesimamishwa kazi kwa muda wakati uchunguzi wa suala hilo ukiendelea.

Mume wa bi Laura amesema kuwa ana mpango wa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya madaktari hao.

source nifahamishe

'Osama Bin Laden ni Kibaraka wa Marekani' - Fidel Castro

Tuesday, August 31, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Osama bin Laden ni kibaraka wa Marekani ambaye anatumiwa na serikali ya Marekani kama njia ya kutoa vitisho vyake, hayo yalisemwa na rais mstaafu wa Cuba, Fidel Castro.
Rais mstaafu wa Cuba, Fidel Castro amesema kuwa Osama bin Laden anafanya kazi CIA na alikuwa akitumiwa na rais wa zamani wa Marekani, George Bush kutangaza vitisho vyake duniani.

Castro alisema kuwa wakati wowote ambao Bush alitaka kutoa vitisho kwa nchi yoyote alimtumia Osama bin Laden kama sababu.

Castro alisema kuwa amejua hayo kwakuwa ameona ushahidi wa maandiko uliotolewa na taasisi ya WikiLeaks ambayo imejipatia umaarufu duniani kwa kutoa taarifa za mambo yaliyofanywa siri.

Castro aliyasema hayo wakati akiongea na mwandishi wa habari wa Lithuania, Daniel Estulin, ambaye anajulikana kwa kuzifanyia uchunguzi taarifa zenye utata.

"Osama anafanya kazi chini ya ikulu ya Marekani, Bush alikuwa na sapoti ya Osama wakati wote", alisema Castro.

"Wakati wowote ambao Bush alitaka kutoa vitisho duniani, alitoa hotuba kuhusiana na Bin Laden akimtaja kuwa anafanya mipango kufanya matukio ya kigaidi".

Castro alisema kuwa maelfu ya kurasa za WikiLeaks zimeweka wazi Al-Qaida wanamfanyia nani kazi.

"Aliyetuthibitishia kuwa Bin Laden ni kibaraka wa CIA ni WikiLeaks, wametoa nyaraka za kuthibitisha hivyo", alisema Castro bila ya kutoa maelezo zaidi kuhusiana na madai yake hayo.

source nifahamishe

Mapenzi Yanapozidi....

Tuesday, August 31, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mfanyabiashara mmoja wa nchini Italia ambaye hakuweza kustahimili kupigwa kibuti na mpenzi wake, ametumia kiasi cha pesa sawa na Tsh. Milioni 30 kutengeneza toy ambalo linafanana kila kitu na mpenzi wake.
Mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 50, hakuweza kuvumilia kukimbiwa na mpenzi wake kiasi cha kuamua kutafuta mpenzi mpya wa bandia ambaye atakuwa naye maisha yake yote.

Mfanyabiashara huyo alitumia kiasi cha dola za kimarekani 18,000 kutengeneza doli la ngono (sex doll) ambalo lilifanana na mpenzi wake wa zamani kuanzia sura, macho mpaka kucha.

Mfanyabiashara huyo alichukua picha kadhaa za mpenzi wake huyo wa zamani na kumwambia mtengeneza madoli wa nchini Italia Diego Bortolin kuwa anataka atengenezewe doli ambalo litafanana na mpenzi wake isipokuwa liwe na matiti makubwa zaidi.

Bortolin alikataa kutaja jina la mfanyabiashara huyo lakini alisema kuwa hutengeneza madoli ya ngono ambayo hukaribia uhalisia ambayo huuzwa kwenye duka lake linaloitwa "Tentazioni" lililopo kwenye mji wa Treviso nchini humo.

"Alitaka mpenzi wake mpya awe na matiti makubwa na makalio makubwa", alisema Bortolin.

Kwa kawaida Bortolin huuza madoli anayoyatengeneza kwa dola 5,000 lakini dili hili la mfanyabiashara liligharimu pesa nyingi kwakuwa lilitakiwa lifanane kila kitu na mpenzi wake kuanzia sura, mpangilio wa meno mpaka kucha.

"Watu wataona kama amefanya kitu cha kipuuzi lakini mimi naona amepata mpenzi mpya mrembo wa maisha", alisema Bortolin.

Doli hilo lina uzito wa kilo 58 na urefu wa mita 1.6. "Ataweza kulikunja na kuliweka katika staili yoyote ile aitakayo", alimalizia kusema Bortolin.


source nifahamishe