Rais aomba wafanyakazi wasitishe mgomo

Friday, April 02, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


RAIS wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amewaomba wafanyakazi wote nchini kusitisha mgomo ambao wameuandaa kupitia shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi na kuwaahidi madai hayo yatafanyiwa kazi.
Rai hiyo ameitoa jana katika hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi ya kungea na wananchi kwa kupitia njia ya vyombo vya habari vyfote nchini.

Ameitaka TUCTA kufikiri zaidi uamuzi huo na kusema mgomo huo utaathiri katika nyanja zote nchini.

Pia amekiri inamuwia vigumu kuzungumzia migomo hiyo kwa wakati na ameeleza kuwa serikali haipuuzi madai ya wafanyakazi wanawajali na wanawathamini.

Hivyo ameitaka TUCTA kukubali kufanya mazungumzo na serikali na waajiri wengine ili kumaliza mgogoro huo ambao hautajenga nchi bali itabomoa.

Mgomo huo unatarajiwa kuanza Mei 5, mweaka huu ambao unalenga mgomo wea wafanyakazi wote nchini kudai madai dambayo hayatekelezwi kwa muda mrefu na serikali.

Tayari vyama kadhaa vinavyounda shirikisho hilo vimeshatangaza kuunga mkono mgomo huo, ambao Kikwete amesema kama utafanyika "shughuli zote nchini zinazofanywa na watu walioajiriwa zitasimama kwa muda usiojulikana kuanzia siku hiyo".

TUCTA inataka siku hiyo watu wote walioajiriwa wagome na kwa muda usiojulikana. Tamko hilo linawahusu wafanyakazi wa umma serikalini na katika mashirika ya umma pamoja na wafanyakazi wa sekta binafsi walioajiriwa popote pale mashambani, maofisini, viwandani, majumbani, mahotelini na madereva.

source nifahamishe

Mchungaji Chapombe Asababisha Kasheshe Makaburini

Friday, April 02, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Askofu wa kanisa katoliki nchini Ufaransa ameomba radhi kufuatia kitendo cha mchungaji mmoja wa kanisa hilo kuongoza mazishi makaburini akiwa amelewa na kumtwanga ngumi ya uso mmoja wa waombelezaji.
"Mchungaji Bonaventure aliwasili makaburini akiwa amelewa katika hali ambayo haiendani na tararibu za kanisa", alisema askofu Robert le Gall katika taarifa yake ya kuwaomba radhi familia ya marehemu.

Ndugu wa mwanamke aliyefariki walielezea jinsi walivyomtaka mchungaji huyo ambaye ni raia wa Burkina Faso kuwa hawataki aongoze misa ya mazishi ya ndugu yao kwakuwa alikuwa amelewa sana.

Katika mazishi hayo yaliyofanyika siku ya jumanne katika mji wa Toulouse uliopo kusini magharibi mwa Ufaransa, mchungaji huyo alikubali kuondoka lakini alipotaka kuendesha gari lake mwenyewe, ndugu wa marehemu walijaribu kumzuia kwakuwa alikuwa hajiwezi hata kutembea akianguka chini mara kwa mara.

Kuna wakati mchungaji huyo alidondoka chini na mmoja wa waombelezaji alipojitolea kumuinua mchungaji huyo alimtandika ngumi ya uso, alisema Gerard Tillier ambaye ni kaka wa marehemu.

"Mchungaji gani huyu anakuja kwenye mazishi akiwa amelewa na kuwapiga ngumi waumini wake? ", alisema kaka huyo wa marehemu

source nifahamishe

Duka La Kwanza la Ngono la Kiislamu Lazinduliwa

Wednesday, March 31, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Duka la kwanza la bidhaa za ngono zinazodaiwa kuwa ni 'HALAL' limezinduliwa kwaajili ya waislamu nchini Uholanzi na baadhi ya mashehe wametoa ruhsa ya duka hilo la kwenye internet wakisema kuwa halivunji sheria za kiislamu.
Duka hilo linalodaiwa kuwa duka la kwanza duniani kwaajili ya waislamu wanaohitaji bidhaa za kuchombeza mapenzi yao lilizinduliwa wiki iliyopita.

Ndani ya siku nne za kuzinduliwa kwa mtandao wa tovuti hiyo kulikuwa na jumla ya cliks 70,000, alitamba mmiliki wa tovuti hiyo ya kwanza ya bidhaa za ngono kwaajili ya waislamu, Abdelaziz Aouragh.

Tovuti hiyo inayoitwa "El Asira" kwa maana ya jamii katika lugha ya kiarabu, ilizinduliwa kwa lengo la kuwauzia wanandoa wa kiislamu bidhaa za erotika.

Abdelaziz ambaye ni raia wa Uholanzi mwenye asili ya Moroko alisema kuwa alianzisha duka hilo la kwenye mtandao ili kuwaepusha waislamu kuingia kwenye tovuti zinazouza bidhaa hizo ambazo huweka picha na video za ngono ambazo ni haramu katika uislamu.

Ukurasa wa mbele wa El Asira hauna kitu chochote zaidi ya mstari unaotenganisha wanawake na wanaume, wanawake hutakiwa kuclick upande wao wa kushoto na wanaume huingia upande wa kulia.

Tovuti hiyo ina lugha tatu za kidachi, kiarabu na kiingereza na huuza zaidi mafuta kwaajili ya masaji, mafuta ya kupunguza ukinzani (lubricants) na dawa mbali mbali za malavi davi.

"Kila kinachopatikana humu ni Halal kinaruhusiwa katika uislamu' alisema Abdelaziz na kuongeza kuwa hakuna picha wala video za ngono kwenye tovuti yake.

Tovuti hiyo inaonyesha bidhaa zikiwa zimepigwa picha kwenye maboxi yake.

Abdelaziz alisema kuwa kabla ya kuanzisha duka hilo la kwenye mtandao alipata ushauri toka kwa mashehe mbalimbali na wanazuoni wa Uholanzi na Saudia ambao walimwambia kuwa hakuna sheria ya kiislamu anayoivunja.

"Ili mradi hauzi toys za ngono au vitu kama hivyo, hakuna tatizo lolote", alisema imamu wa Uholanzi, Abdul Jabbar.

"Mtume Muhammad (s.a.w) alitoa ushauri mbalimbali kuhusiana na masuala ya mapenzi kwenye ndoa, hivyo hakuna kitu cha kukionea aibu", aliongeza imamu huyo.

source nifahamishe

Maiti za Watoto Zatupwa Kwenye Mto

Wednesday, March 31, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Wafanyakazi wawili wa monchwari nchini China wanashikiliwa na polisi baada ya kuzitupa maiti 21 za watoto kwenye mto.
Wafanyakazi wawili wa ngazi za juu wa hospitali moja nchini China wamefukuzwa kazi huku wafanyakazi wawili wa monchwari wakiwa mbaroni baada ya maiti 21 za watoto kuopolewa toka kwenye mto.

Maiti za watoto wanane zilikuwa na alama za kuonyesha kuwa zilikuwa zimehifadhiwa kwenye hospitali ya chuo kikuu cha Jining Medical University katika mji wa Shandong, limeripoti shirika la habari la Xinhua.

Taarifa zinasema kuwa maiti za watoto hao zilikuwa ni za vichanga vilivyouliwa wakati wa utoaji mimba na watoto waliofariki kutokana na maradhi mbali mbali.

Taarifa za polisi zinasema kuwa wafanyakazi hao wa monchwari walilipwa na ndugu wa watoto waliofariki wazizike maiti za watoto hao lakini wao waliamua kuzitupa kwenye mto ulio mbali sana na hospitali hiyo.

Maiti za watoto zikiwa katika mifuko ya rambo ya njano ziliopolewa toka kwenye mto na kuzua hasira za wananchi walioshuhudia tukio hilo.


source nifahamishe

Jela Miezi Sita Kwa Kumuonyesha Kidole cha Kati Mwarabu

Wednesday, March 31, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Raia wa Uingereza anayeishi Dubai huenda akatupwa jela miezi sita kwa kosa la kumtukana kwa kumuonyesha kidole cha kati mwanafunzi wa kiarabu toka Iraq.
Simon Andrews, raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 56 anakabiliwa na hukumu ya kwenda jela miezi sita iwapo atapatikana na hatia ya kumuonyesha kidole cha kati mwanafunzi wa urubani toka Iraq.

Gazeti la The Sun la Uingereza limeripoti kuwa Simon alishindwa kuzizuia hasira zake wakati wa ugomvi wake na mwanafunzi Mahmud Rasheed na kuamua kumtukana kwa kumuonyesha kidole cha kati.

Mahmud alikimbilia polisi kupeleka malalamiko yake na haikuchukua muda mrefu Simon alitiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka mahakamani.

Simon amepigwa marufuku kusafiri nje ya Dubai tangia alipotiwa mbaroni mwezi wa nane mwaka jana.

Akitoa ushahidi wake mahakamani siku ya jumapili, Simon alijitetea kuwa hakufanya kitendo hicho na kwamba raia huyo wa Iraq anamsingizia.

Mahmud hakujitokeza mahakamani kutoa ushahidi dhidi ya Simon na pia hakuna mtu aliyejitokeza kama shahidi wa kesi hiyo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi aprili nne wakati uchunguzi zaidi ukiendelea

source nifahamishe

Mwanamke Mwenye Wivu wa Ajabu Ahukumiwa Kifo

Wednesday, March 31, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanamke wa nchini Kuwait ambaye alianzisha moto kwenye harusi kupinga mumewe kuoa mke mwingine na kupelekea vifo vya watu 57 amehukumiwa adhabu ya kifo.
Akitoa hukumu dhidi ya Nasra Yussef Mohammed al-Enezi, 23, jaji Adel al-Sager aliamuru Nasra auliwe kwa kitendo chake cha kuanzisha moto kwenye hema wakati wa sherehe za harusi na kupelekea vifo vya watu 57.

Nasra alipatikana na hatia ya kulichoma moto hema ambalo wanawake na watoto walikuwa wamekaa wakati wa harusi ya mumewe akiongeza mkewe mwingine.

Moto katika tukio hilo la mwezi wa nane mwaka jana, uliwateketeza wanawake na watoto ndani ya dakika 10 tu na ulisababisha majeruhi kadhaa.

Nasra alianzisha moto huo ili kupinga mumewe kuongeza mke mwingine.

Nasra alikamatwa siku moja baada ya wanawake 41 na watoto kufariki kwenye moto uliozuka kwenye hema katika mji wa Jahra uliopo magharibi mwa Kuwait. Idadi ya vifo iliongezeka baadae na kufikia 57.

Awali ilidaiwa kuwa alikuwa amepewa talaka na mumewe lakini wakili wa utetezi walisema kuwa alikuwa bado ni mke wa bwana harusi huyo na alikuwa na mimba ya miezi miwili ambayo mawakili wake wanadai ilitolewa alipokuwa jela.

Nasra na mumewe walikuwa na watoto wawili ambao wote walikuwa na matatizo ya akili.

Mawakili wa Nasra wamesema watakata rufaa ya hukumu hiyo mahakama kuu.
source nifahamishe

Mwanaume Mwenye Matiti Makubwa Kuliko Wote Duniani Agunduliwa China

Monday, March 29, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Madaktari nchini China wanadai kumgundua mwanaume mwenye matiti makubwa kuliko wote duniani.
Madaktari nchini China wanadai kumgundua mwanaume mwenye matiti makubwa kuliko wote duniani baada ya mwanaume huyo kujitokeza kwenye kliniki moja mjini Beijing.

Daktari wa hospitali ya Jinan Chest Hospital, Dokta Zhang Lilan alisema "Huyu ni mwanaume kamili isipokuwa ana matiti kama mwanamke".

"Yeye ni mkulima na anasema kuwa anasumbuliwa na ukubwa wa matiti yake wakati anapofanya kazi zake za kilimo".

"Anasema pia matiti yake yamekuwa gumzo kijijini kwake ambapo watu wengi wamekuwa wakimtafuta ili kumuona na imekuwa kero kubwa sana kwake kiasi cha kumfanya awe anavaa makoti makubwa hata wakati wa joto kali ili kuyaficha matiti yake", alisema dokta Lilan.

Mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Guo Feng mwenye umri wa miaka 53, alisema "Miaka 10 iliyopita matiti yangu yalianza kuwa makubwa lakini nilikuwa nikifikiria unene wangu ndio sababu .. lakini miaka michache iliyopita nimekuwa nikizunguka hospitali moja baada ya nyingine kutafuta tiba lakini hakuna mtu anayetaka kunisaidia".

"Nimetumia pesa nyingi sana kwenye vipimo hospitalini lakini hakuna jibu lolote la maana huku matiti yangu yakiendelea kuwa makubwa", alisema Guo Feng.

"Wakati mwingine huwa nafikiria madaktari hawataki kunisaidia", alilamika Guo Feng.

Dokta Lilan alisema kuwa Guo Feng ametishia kuyakata matiti yake yeye mwenyewe iwapo hakuna daktari atakayejitokeza kumpatia tiba.

Hata hivyo madaktari wamekataa kuchukua hatua yoyote mpaka watakapogundua sababu ya matiti yake kuwa na ukubwa huo usio wa kawaida.

"Katika miaka yangu 30 ya kufanya kazi ya udaktari sijawahi kukumbana na kitu kama hichi", alisema Dokta Lilan.

"Awali tulidhania amekula kitu chenye sumu lakini vipimo vya damu yake havijaonyesha kitu chochote. Tumemfanyia X-ray hana dalili ya kansa", aliongeza mmiliki wa hospitali hiyo

source nifahamishe