Unga Unawamaliza Wasanii wa Bongo Flava

Sunday, November 08, 2009 / Posted by ishak / comments (0)


Muziki wa kizazi kipya Bongo Flava uko hatarini kutokana na kwamba mastaa wake wengi ambao wamewahi kutamba katika fani hiyo wanaanza kupotea mmoja mmoja baada ya kupata pesa na kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.
Unga unaimeng’enya Bongo Flava
Mambo hayapo ok, Bongo Flava inazidi kumeng’enywa na nguvu kazi yake inapungua. Hapa ni gumzo kuwa vijana wengi wapo kwenye skendo ya kutumia dawa za kulevya.

Kuna maswali magumu; Kwanini baadhi ya wasanii wana-shine kidogo, wanakubalika kitaa na kiasi fulani maisha yao kuwa bora lakini ghafla tu madogo wanaonekana kitaa wamechoka na afya zimekuwa dhaifu.

Madai ya msingi ni matumizi ya dawa za kulevya a.k.a unga, kwamba madogo wengi wakishakubalika kitaa kwa njia moja au nyingine hujiingiza kwenye matumizi ya unga, wanabwia na wengine wanajidunga kabisa.

Its dangerous! The only gent on kundi marehemu la Wakilisha, Langa Kileo anaweza kuwa mfano hai, baada ya kukiri kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa iliyopita kuwa alikuwa anabwia unga lakini sasa amestop. Langa alisema kuwa alikuwa mbwiaji mzuri wa Cocktail kabla ya hivi karibuni kuugua typhoid, hivyo kukosa access ya kupata unga.

Alisema, alianza kama utani lakini baadaye alizidiwa na akawa hawezi kuacha, ingawa sasa hivi anamshukuru Mungu kwamba yamepita. Katika hilo, Langa alieleza kwamba angalau sasa anajisikia nafuu na afya imeanza kurejea. Hiyo ni kauli ya Langa kupitia session ya Crazy Friday, lakini ukweli ni kuwa madogo kibao wapo kwenye skendo ya kubwia.

Albert Mangwea ‘Ngwair’, Heri Samir ‘Blu’ Mark II B a.k.a Simba ni kati ya majina ambayo yanatajwa kwenye orodha ya wanaodaiwa kubwia unga. Hayo ni majina yanayotajwa lakini nyuma ya pazia ni wengi na hii inasababisha kizazi kipya kisiwe na afya standard. Madogo wanasimama vizuri lakini baadaye wanakuwa dhoofu l’hali. Hii ni hatari na sisi kama wadau tunalaani vikali matumizi ya dawa za kulevya.

source.nifahamishe

Jambazi Anapowatumia Polisi Picha Yake...

Sunday, November 08, 2009 / Posted by ishak / comments (0)


Jambazi anayetafutwa na polisi kila kona nchini Uingereza amewatumia polisi picha yake mpya aliyopiga akiwa mbele ya gari ya polisi baada ya kuchukizwa na picha yake ambayo polisi waliitoa kwenye magazeti wakiomba wananchi wawasaidie kumnasa.
Jambazi Matthew Maynard mwenye umri wa miaka 23 hakuipenda picha yake iliyotolewa kwenye magazeti na aliamua kuwatumia polisi picha yake mpya aliyopiga akiwa mbele ya gari la polisi.

Polisi katika mji wa Swansea walitoa tangazo la kutafutwa kwa Matthew katika gazeti la Evening Post la mji huo. Tangazo hilo liliambatana na picha yake ndogo inayoonyesha sura yake.

Baada ya picha hiyo kuchapishwa kwenye gazeti hilo, Matthew ambaye pamoja na wenzake wanne wanatafutwa na polisi kwa makosa ya ujambazi, alipiga simu kwenye ofisi ya gazeti hilo akisema kuwa hajaipenda picha yake iliyotolewa kwenye gazeti hilo na aliwaahidi atawatumia picha nyingine waiweke kwenye gazeti lao.

Wakati waandishi wa gazeti hilo wakiwa hawaamini kama kweli atawatumia picha yake, Matthew alitumia simu yake kuwatumia picha yake aliyopiga akiwa mbele ya gari la polisi akiwa amevaa jaketi linalofanana na majaketi wanayopenda kuvaa mapolisi.

Picha yake hiyo ilitolewa juzi kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti la Evening Post.

Jana polisi wa Swansea walimshukuru Matthew kwa kuwasaidia polisi katika harakati zao za kumtia mbaroni.

"Anajiona mjanja sana kwa kujionyesha namna hii, tutamnasa muda si mrefu", alisema afisa mmoja wa polisi.

"Watu wote wa Swansea wanajua sasa jinsi alivyo na watatupa taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwake".

"Kama ana akili angejisalimisha mwenyewe polisi sasa kwakuwa hana pa kukimbilia tena", alimalizia kusema afisa huyo.

source.nifahamishe.com

CUF yamtambua Rais Karume, Maalim Seif Hamad Nusura Ashushiwe Kipigo

Sunday, November 08, 2009 / Posted by ishak / comments (0)


Katibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani katika siasa za visiwa vya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad alitangaza jana kumtambua rais Karume kama rais halali wa Zanzibar na kusababisha hasira toka kwa wafuasi wa CUF ambao almanusura wamshushie kipigo wakidai viongozi wa CUF wamewasaliti.
Akiongea katika mkutano wa hadhara katika uliofanyika kwenye viwanja vya Kibandamaiti, Maalim Seif Hamad alizomewa na kulazimika kushuka toka kwenye jukwaa akiwa chini ya ulinzi mkali baada ya kutangaza kuwa CUF imeamua kumtambua Rais Amani Abeid Karume.

Akiongea katika mkutano huo, Maalim Seif Hamad alisema kwamba baraza kuu la uongozi wa CUF limefanya kikao na kuamua kumtambua rais Amani Abeid Karume kama rais halali wa Zanzibar ili kumaliza msukosuko wa kisiasa katika visiwa hivyo.

Tamko hilo la Maalim Seif limefuatia kikao chake na rais Karume ndani ya ikulu ya Zanzibar na kisha kufuatiwa na mkutano wa baraza la kamati kuu ya chama hicho.

Maalim Seif alisema kuwa uamuzi huo ulikuwa ni mgumu kufanywa kwa vile chama hicho kimekuwa kikiibiwa kura zake katika uchaguzi kila uchaguzi unapofanyika visiwani humo.

Uamuzi huo wa Maalim Seif kumtambua rais Karume uliamsha hasira za wafuasi wa CUF ambao walianza kumzomea huku wakipiga kelele "hatukubali hatukubali".

Kutokana na vurugu iliyoanza kuzuka kwenye mkutano huo ambapo baadhi ya wafuasi wa CUF walianza kutembea kuelekea kwenye jukwaa hilo, ilibidi Maalim Seif alazimike kushuka jukwaani na kupewa ulinzi mkali kunusuru maisha yake na kwenda kukaa kwenye jukwaa la viongozi wa CUF.

Baada ya hapo mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba alipanda jukwaani kujaribu kuwatuliza wafuasi wenye hasira ambao waliwaona viongozi wao kama wasaliti na wengine kuangua kilio.

Hata hivyo hali haikutulia na wafuasi wa chama hicho walianza kupiga kelele za kuwataka viongozi wa chama hicho wajiuzulu.

Wafuasi hao walilalamika kuwa baadhi yao na ndugu zao wamepoteza maisha na wengine kuwa vilema kwa sababu ya kutetea siasa za chama hicho na matokeo yake chama hicho kimewasaliti.

Chama cha CUF kwa miaka kadhaa sasa katika chaguzi za mwaka 1995, 2000, na 2005 kimekuwa kikigoma kuitambua serikali na baadhi ya nyakati wajumbe wake wa baraza la wawakilishi waligoma kuingia vikaoni.

Miongoni mwa mazungumzo ya kutafuta muafaka yaliyofanyika mwezi Februari mwaka huu, yalikwama baada ya CUF kukataa kumtambua rais Karume kama rais halali wa Zanzibar na kwa upande wake rais Karume aligoma kuwachagua wajumbe wawili wa CUF kuingia katika baraza la wawakilishi kwa sababu hiyo hiyo.

Ukiwa ni mwaka mmoja tu umebakia kufanyika kwa uchaguzi mwingine mkuu visiwani humo, baadhi ya wataalamu wa siasa za Zanzibar wanadhani CUF itapita katika kipindi kigumu huku wengine wakiamini kuwa uamuzi wa kusamehe dhuluma wanzodai kufanyiwa unaweza kukifanya chama hicho kuwa imara zaidi visiwani humo.

source.nifahamishe.com