Hatari Tunayoichekelea

Wednesday, May 05, 2010 / Posted by ishak /

Ile fainali ya mchezo wa kiduku ambao wanaume huvaa nguo za kike wakishindana kukatika mauno kama wanawake imefanyika na muaandaji wa mashindano hayo amepongezwa kwa kuwaletea wabongo ubunifu mpya ingawa baadhi ya wadau wanahofia mchezo huo utawaharibu vijana.
Ilikuwa ni usiku ambao kusema kweli nilisikitika kumuona mwanaume akiwa amevaa sidiria na gagulo akikatika viuno kama mwanamke.

Kijana mwingine naye bila haya aliyabenua makalio yake kumuelekezea mwenzake huku akikata mauno ambayo yalinifanya nijiulize wapi tunawapeleka vijana wa taifa la kesho.

Hiyo ilikuwa ni sehemu ya vionjo vya fainali ya kiduku ambapo vijana wa kitanzania walishindana kukata mauno kuwania dola 250.

Katika fainali hiyo kundi la Visqua toka kiwalani ndilo lililowashinda wenzao kwa mauno na kutunukiwa dola 250.

Mamia ya watu walifurika kwenye ukumbi wa Travertine, Magomeni kushuhudia fainali hizo.

Ingawa baadhi ya wadau wanauona mchezo wa kiduku kama vile unawahatarisha vijana kugeuka kuwa mashoga, muandaaji wa mashindano hayo Maimartha wa Jesse alipongezwa sana na kusifiwa kwa ubunifu wake wa kutuletea watanzania mchezo mpya aliouita kiduku.

Wiki mbili zilizopita niliwaletea picha za hatua ya awali ya mashindano ya Kiduku na wadau wengi walikasirishwa na wanafunzi wakiwa katika unifomu za shule kushiriki kwenye mashindano hayo.

Vijana wengine walionekana wakiwa wamevaa vipande viwili vya kanga hali iliyowafanya watu wengi waweke maswali ya kuuliza muandaaji wa kiduku ana malengo gani.

Hata hivyo Mgeni rasmi wa fainali za kiduku zilizofanyika jumamosi alikuwa mbunge wa Kinondoni, Mh. Iddi Azzan wakati viongozi wa klabu ya Simba walikuwa wageni waalikwa na walikuja na kombe lao la ligi kuu ya bara walilolitwaa wiki chache zilizopita.

source nifahamishe