Ajirusha Uchi Toka Ghorofa ya 11

Thursday, August 12, 2010 / Posted by ishak /


Wakati China ikiendeleza kuombeleza vifo vya mamia ya watu kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo, mwanamke mmoja nchini humo amejaribu kujiua kwa kujirusha toka ghorofa ya 11 huku akiwa uchi wa mnyama.
Kufuatia mzozo na mumewe, mwanamke mmoja wa nchini China alijaribu kusitisha maisha yake kwa kujirusha toka ghorofa ya 11.

Katika tukio hilo lililotokea kwenye jimbo la Anhui nchini humo, mwanamke huyo alisababisha kizaazaa baada ya kuvua nguo zake zote na kupanda kwenye dirisha la nyumba iliyopo ghorofa ya 11 na kutishia kujiua kwa kujirusha chini.

Pamoja na jitihada za zimamoto na majirani kumsihi asijirushe, mwanamke huyo aliamua kujirusha ili kuhitimisha maisha yake.

Hata hivyo maisha ya mwanamke huyo yalinusurika baada ya kuangukia kwenye boya lililowekwa chini na zimamoto. Aliwahishwa hospitali kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Iligundulika kuwa sababu ya mwanamke kujaribu kujiua ni mzozo uliotokea usiku wa siku moja kabla ya tukio hilo.


source nifahamishe