Mwanaume Mjamzito' Kujifungua Mtoto wa Tatu

Sunday, August 01, 2010 / Posted by ishak /


Thomas Beatie ambaye mwaka 2008 alikuwa gumzo duniani akitambulika kama mwanaume wa kwanza duniani kupata ujauzito anatarajiwa kujifungua mtoto wa tatu muda wowote kuanzia sasa.
Mwanamke aliyebadilisha jinsia na kuwa mwanaume na kisha kutambulika kama mwanaume wa kwanza duniani kupata ujauzito, anatarajiwa kujifungua mtoto wa tatu.

Thomas Beatie, alijifungua mtoto wake wa kwanza aliyepewa jina la Susan mwezi juni mwaka 2008 na mwaka mmoja baadae alijifungua mtoto mwingine aliyepewa jina la Austin.

"Ameishatimiza muda wake wa kujifungua na ameipita siku aliyotarajiwa kujifungua", alisema mdau mmoja wa karibu na familia hiyo.

Thomas alizaliwa kama mwanamke akijulikana kwa jina la Tracy lakini mwaka 2002 alianza kutumia madawa ya homoni kubadilisha jinsia yake kuwa mwanaume lakini hakufanya operesheni ya kuzibadilisha sehemu zake za siri.

Umbile lake lilibadilika na kufanana na mwanaume huku akifuga madevu ili aonekane kama mwanaume kweli.

Alibadilisha kisheria jinsia yake kuwa mwanaume na jina lake alilibadili kuwa Thomas badala ya Tracy.

Mwaka 2003 alifunga ndoa na mwanamke aliyeitwa Nancy ambaye alikuwa ni mama wa watoto wawili aliyepewa talaka na mumewe.

Baada ya kugundua kuwa Nancy hawezi kupata ujauzito tena kutokana na umri wake, Thomas aliamua kushika ujauzito kwa njia ya upandikizaji ili familia yake iweze kupata mtoto.

Huo ndio ulikuwa mwanzo wa Thomas kujulikana duniani kama mwanaume mjamzito. Alipata mtoto wa kwanza mwaka 2008 na sasa anatarajia kupata mtoto wa tatu.


source nifahamishe