Apata Mimba Sita Nje ya Ndoa, Awaua Watoto na Kuficha Maiti

Thursday, October 28, 2010 / Posted by ishak /


Mwanamke wa nchini Marekani ambaye alipata mimba sita nje ya ndoa bila ya mume wake kujua, aliwaua watoto wake na kuzificha maiti zao kwenye sanduku.
Michele Kalina mwenye umri wa miaka 44 mkazi wa Pennsylvania nchini Marekani, alizificha mimba sita alizozipata kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa na aliwaua watoto wote waliotokana na mimba hizo na kuzificha maiti zao kwenye masanduku.

Matokeo ya DNA yalionyesha kuwa mifupa ya binadamu iliyokutwa kwenye sandaku lililotiwa kufuli ilikuwa ni mifupa ya watoto watano ambapo wanne kati ya watoto hao walizaliwa wakiwa hai wakati mmoja alizaliwa akiwa tayari ameishafariki.

Kalina na mumewe wa ndoa, Jeffrey walifanikiwa kupata watoto wawili, mmoja wa kike mwenye umri wa miaka 19 na mwingine wa kiume ambaye aifariki dunia mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 13.

Mahakama ilithibitisha kuwa watoto wanne kati ya sita Kalina alizaa na kibuzi chake nje ya ndoa.

Mume wa Kalina na binti yake waligundua mifupa ya watoto wachanga ikiwa imefichwa kwenye maboksi ndani ya sanduku mwezi wa nane mwaka huu ambapo waliripoti polisi na Kalina alitiwa mbaroni.

Mume wa Kalina aliwaambia polisi kuwa ni mara moja tu alihisi mke wake alikuwa mjamzito lakini hakuwa na uhakika.

Mwanaume aliyekuwa akijiiba na Kalina ambaye jina lake liliwekwa kapuni, aliwaambia polisi kuwa Kalina alimwambia kuwa alikuwa na uvimbe tumboni uliolifanya tumbo lake liwe kubwa na uvimbe huo ulikuwa ukimtokea mara kwa mara.

Mwanaume huyo naye alisisitiza kuwa hakugundua kama Kalina alikuwa mjamzito.

Kalina ametupwa jela akikabiliwa na makosa ya mauaji na kuficha maiti za watoto wake.

Kesi ya Kalina itaanza kusikilizwa wiki hii.

source nifahamishe