Tamaa ya Umaarufu Yapelekea Aiage Dunia

Sunday, January 23, 2011 / Posted by ishak /


Mwanamke nyota wa filamu za ngono wa nchini Ujerumani ambaye alijipatia umaarufu mkubwa baada ya kushiriki 'Big Brother Germany' amefariki dunia baada ya operesheni ya sita ya kurekebisha matiti yake ili jina lake liendelee kutamba kwenye vyombo vya habari.
Carolin Berger mwenye umri wa miaka 23 ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na ushiriki wake kwenye mashindano ya "Big Brother Germany", amefariki dunia kutokana na matatizo ya kiafya aliyopata baada ya operesheni ya sita ya kuongeza ukubwa wa matiti yake.

Carolin ambaye awali alikuwa akishiriki kwenye sinema za ngono akijulikana kwa jina la Cora kabla ya kushiriki kwenye mashindano ya Big Brother alitaka jina lake liendelee kutamba kwenye vyombo vya habari.

Carolin alifariki juzi muda mfupi baada ya kumalizika kwa operesheni yake ya sita ya kuongeza ukubwa wa matiti yake.

Carolin aliongeza ukubwa wa matiti yake toka saizi 34F hadi 34G.

Alikumbwa na mashambulio ya moyo mara mbili, presha ilishuka ghafla na ubongo wake ulipata madhara makubwa na mwishoe aliiaga dunia.

Daktari aliyemfanyia operesheni hiyo anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.


source nifahamishe