MAHAKAMA ya Wilaya yaMwanakwerekwe Mjini Zanzibar imemuhukumu kifungo cha miaka miwili jela pamoja na kulipa fidia ya shilingi 200,000/ Ramadhan Tuma (28) kwa kosa la kuchoma moto kitabu kitakatifu kiitwacho msahafu. Hukumu hiyo imetolewa mahakamani hapo na Hakimu Khamis Ali Simai baada ya kuridhika na na ushahidi na kupatikana na hatia hiyo.
Hakimu Simai alisema kuwa,upande wa mashitaka umeweza kuthibitisha makosa hayo dhidi ya mtuhumiwa na atapewa adhabu hiyo kwa mujibu wa sheria kwa kuwa kitendo hicho ni uvunjifu wa amani kwa mujibuwa sheria za Zanzibar.
Kabla ya kutolewa hukumu hiyo mtuhumiwa aliiomba mahakama hiyo impunguziwe adhabu kwa madai kuwa ana familia inayomtegemea akiwemo mke na mtoto pia aliiambia mahakama kuwa alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya tumbo ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.
Awali ilidaiwa kuwa, Ramadhan Handa Tuma alifanya kosa hilo Novemba 16, mwaka jana, akiwa hadharani kwa makusudi alichoma moto kitabu kitakatifu cha dini ya kiislamu ‘msahafu’ pamoja na juzuu.
source nifahamishe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment