Azichoma Moto Sehemu za Siri za Mpenzi Kwa Kumhisi Anatembea Nje

Monday, January 17, 2011 / Posted by ishak / comments (0)Mwanamke mmoja mwenye wivu sana wa nchini Marekani amefikishwa mahakamani baada ya kuzichoma moto sehemu za siri za mpenzi wake baada ya kushuku kuwa mpenzi wake huyo ana kimada nje.
Victoria Bynes mwenye umri wa miaka 29, wa Florida nchini Marekani alichukua mafuta ya petroli na kumwagia kwenye sehemu za siri za mpenzi wake kabla ya kutumia kiberiti kuwasha moto uliozitekeza sehemu nyeti za mpenzi wake.

Wakati mpenzi wake, Andrew Williams akihangaika kuuzima moto uliokuwa ukizitekeza sehemu zake muhimu za kiume, Victoria alipanda kwenye gari lake na kuondoka bila ya kutoa msaada.

Wakati polisi walipofika walimkuta Andrew akiwa ameungua vibaya sehemu zake za siri pamoja sehemu za tumbo lake.

Sababu ya Victoria kuzichoma moto nyeti za mpenzi wake ni kumshuku kuwa ana mwanamke mwingine kwakuwa alishindwa kuwasiliana naye kwa muda wa wiki moja.

Majirani walisema kuwa Victoria alifika kwenye nyumba ya Andrew na punde walianza kulumbana kwa sauti.

Wakati wa malumbano hayo, Victoria aliitikisa chupa yenye mafuta ya petrol aliyokuja nayo na kumwagia mpenzi wake kwenye sehemu zake nyeti na kisha kuwasha moto kwa kutumia kiberiti alichokuja nacho.

Victoria akijitetea alisema kuwa alizipiga moto nyeti za mpenzi wake kwa bahati mbaya kwakuwa lengo lake lilikuwa ni kumtishia kuzichoma moto nyeti zake.

Victoria aliachiwa huru kwa dhamana ya dola 10,000 wakati uchunguzi wa kesi hiyo ukiendelea.

Andrew bado amelazwa hospitali akipatiwa matibabu kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata kwenye nyeti zake na tumboni.

Tukio hili limetokea ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya mwanamke mwingine naye wa Florida, kuzichoma moto sehemu za siri za mpenzi wake, baada ya kutokea mzozo kati yao.

Berlinda Dixon-Newbold alitiwa mbaroni mwezi disemba mwaka jana kwa kuzichoma moto sehemu za siri za mpenzi wake Sheldon Gonzales.

Katika tukio jingine huko huko Marekani katika jimbo la Kansas, Mwanamke mwenye umri wa miaka 42, alimpiga risasi kwenye sehemu za siri mumewe mwenye umri wa miaka 50 kutokana na malumbano ya ndani ya nyumba.

Mwanamke huyo bado anashikiliwa na polisi kwa kitendo chake hicho.

source nifahamishe