Ruhsa Kumpiga Mkeo Lakini Usimtoe Alama

Thursday, October 21, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mahakama ya sheria za kiislamu katika falme za kiarabu UAE imeamuru kuwa ni ruhsa mwanaume kumpiga mkewe na watoto wake ili mradi hatasababisha alama za vipigo kwenye miili yao.
Hatua hiyo ya mahakama hiyo inawapa haki za kisheria wanaume kuwaadhibu wake zao na watoto wao iwapo wataenda kinyume na matakwa yao.

Hukumu hiyo ilitolewa na mmoja wa majaji wakuu wa UAE, Falah al Hajeri, ambaye alikuwa akitoa hukumu ya mwanaume aliyepigwa faini sawa na Tsh. 160,000 kwa kumpiga kibao mkewe na kumpiga teke binti yake.

Mwanaume huyo alipatikana na hatia ya kumpiga mkewe kwa nguvu sana kiasi cha kusababisha apasuke mdomo wake na kuvunjika jino lake.

Mwanaume huyo pia alimpiga mateke binti yake mwenye umri wa miaka 23 kiasi cha kupelekea apate michuko na uvimbe kwenye mguu na mkono wake.

Mwanaume huyo ambaye jina lake liliwekwa kapuni, awali alidai alimpiga mkewe na mtoto wake kwa bahati mbaya lakini alipopatikana na hatia alikata rufaa akisema kuwa hata kama alimpiga mkewe na mtoto wake kwa makusudi, anayo haki kwa mujibu wa sheria za kiislamu kutumia nguvu dhidi yao iwapo njia zingine za kuwaadabisha zitakuwa zimefeli.

Akitoa hukumu ya kesi hiyo, jaji Falah al Hajeri alisema: “Ingawa sheria zinaruhusu waume kuwapiga wake zao, lakini pia wanatakiwa wasivuke mipaka na kusawasababisha alama au makovu wake zao”.

“Kama mume atakiuka misingi ya sheria ya kumuadhibu mke au mtoto wake, basi lazima ahukumiwe kwa mujibu wa sheria”, alisema jaji Hajeri.

Jaji Hajeri alielezea kuwa njia rahisi ya kuangalia kama waume wavunja sheria ya kuwaadhibu wake zao ni kwa kuangalia alama za vipigo kwenye miili ya wake zao.

source nifahamishe

Kaka Yake Obama Aoa Mwanafunzi Aliyemtorosha Kwao

Sunday, October 17, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Kaka wa kufikia wa rais wa Marekani, Barack Obama anayeishi nchini Kenya, Malik Obama mwenye umri wa miaka 52 ameongeza mke wa tatu ambaye ni mwanafunzi wa sekondari mwenye umri wa miaka 19 aliyeacha shule na kukimbia kwao.
Kaka wa kufikia wa rais wa Marekani, Barack Obama anayeishi nchini Kenya, Malik Obama ambaye ana wake wawili ameongeza mke wa tatu ambaye ni mwanafunzi wa sekondari aliyekimbia masomo yake.

Mama wa msichana huyo mwenye umri wa miaka 52, alielezea hasira zake baada ya binti yake kuacha masomo ili aolewe na Malik ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 52.

Akiongea na televisheni ya NTV ya Kenya, mama wa msichana huyo anayeitwa Mary Aoko Ouma alisema kuwa binti yake awali alijaribu kufunga ndoa na Malik miaka miwili iliyopita lakini hakumruhusu.

Akiongea na televisheni ya NTV bila ya kujua kuwa anarekodiwa, Malik alithibitisha kufunga ndoa na msichana huyo ingawa hakusema ni lini harusi yao ilifanyika.

Sheria za Kenya zinaruhusu mtu kuoa mke zaidi ya mmoja iwapo vigezo vya kidini au kitamaduni vitatumika.

source nifahamishe

Babu Nyota wa Video za Ngono

Saturday, October 09, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Babu mwenye umri wa miaka 76 wa nchini Japan alikuwa akitoka nyumbani kwake kila siku asubuhi akiwa ameuramba suti akiaga anaenda kazini lakini siri yake imegundulika kuwa babu huyo alikuwa akitoka nyumbani kwake asubuhi ili kwenda kushiriki video za ngono.
baada ya kustaafu kazi yake ya uwakala wa kampuni ya utalii, babu Shigeo Tokuda, mwenye umri wa miaka 76 alikuwa akiiaga familia yake aubuhi kuwa anaenda kazini.

Familia yake haikuwa ikijua babu Tokuda alikuwa akienda wapi na alikuwa akifanya kazi gani mpaka hivi karibuni ilipogundulika kuwa babu Tokuda ndiye mwanaume mzee kuliko wote nchini Japan anayeshiriki kwenye video za ngono.

Tokuda aligundulika kuwa ni nyota wa video za ngono baada ya binti yake mwenye umri wa miaka 35 kusoma jarida ambalo lilikuwa likimuelezea babu Tokuda kama mfalme wa filamu za kiutu uzima.

Baada ya kuona familia yake imegundua kazi yake mpya anayoifanya, Tokuda aliamua kuweka wazi kwa kutoboa siri zote.

Tokuda alisema kuwa alipokuwa na umri wa miaka 60, alikutana na mtengenezaji wa filamu za ngono wakati akiwa dukani akinunua DVD ya ngono. Huo ndio ukawa mwanzo wa yeye kujiingiza kwenye filamu za ngono.

Hadi sasa Tokuda ameishashiriki jumla ya filamu 350 za ngono na amekuwa akilipwa kiasi cha dola 500 kila siku.

Tokuda ambaye ana mjukuu mmoja alisema kuwa mkewe ameiridhia kazi yake mpya ingawa binti yake alishtushwa sana alipogundua kuwa yeye ni nyota wa video za ngono.


source nifahamishe

Bikira Kuwa Sharti la Kuingia Shule za Sekondari

Friday, October 01, 2010 / Posted by ishak / comments (0)

Wasichana waliopoteza bikira zao hawatapata nafasi za kujiunga na shule za sekondari za serikali nchini Indonesia iwapo muswada mpya wa sheria wa kuzuia vijana kuanza uzinzi mapema utapitishwa na bunge la nchi hiyo.
Muswada wa sheria umefikishwa bungeni nchini Indonesia ukitaka wasichana waliopoteza bikira zao wasiruhusiwe kujiunga na shule za sekondari nchini humo.

Muswada huo wa sheria umetolewa na mbunge wa jimbo la Jambi nchini humo Babang Bayu Suseno ambaye ameeleza kuwa muswada huo ukipitishwa kuwa sheria utasaidia kuzuia vijana kuanza uzinzi mapema.

Suseno alisema kuwa upatikanaji wa video na picha za ngono na ufahamu mdogo wa masuala ya dini umepelekea vijana kujihusisha na matendo ya ngono mapema.

Mbunge huyo ametaka wanafunzi wa kike wafanyiwe uchunguzi kuthibitisha bikira zao kabla ya kuruhusiwa kuingia shule za sekondari za serikali.

Hata hivyo muswada huo umekumbwa na upinzani mkubwa toka kwa wanasiasa na taasisi za kutetea haki za binadamu.

Imeelezwa kuwa kuwalazimisha wasichana kupima bikira zao itakuwa ni kuwabagua na ni kinyume cha haki za binadamu.

"Njia ya kuzuia uzinzi kwa vijana ni kwa kuwapa elimu ya masuala ya jinsia", alisema Seto Mulyadi, mkuu wa kitengo cha taifa cha kuwalinda watoto na kuongeza "Sio wasichana wote wanaoshiriki kwenye masuala ya ngono wanafanya hivyo kwa kupenda".

"Weka somo maalumu shuleni la kuwafundisha wanafunzi jinsi ya kujilinda lakini sio kuwapima bikira", aliongeza Mulyadi.

Indonesia ni nchi yenye waislamu wengi kuliko wote duniani wapatao milioni 210. Wengi wao wana msimamo wa kati lakini wale wenye msimamo mkali wanahofia kuwa maendeleo ya kasi yanayoambatana na vijana kuiga umagharibi yanapelekea kupungua kwa msimamo wa kidini nchini humo.

Ili muswada huo upitishwe inabidi upewe sapoti ya gavana wa jimbo la Jambi pamoja na waziri wa masuala ya wanawake, lakini viongozi hao wawili ndio waliokuwa wa mwanzo kuupinga muswada huo.

source nifahamishe

Ajiua Baada ya Video Akilawitiwa Kuwekwa Online

Friday, October 01, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanafunzi wa kiume wa nchini Marekani ambaye marafiki zake walirekodi kwa siri video wakati akiingiliwa kinyume cha maumbile na mwanaume mwenzie na kisha kuiweka video hiyo kwenye internet amejiua kwa kujirusha toka kwenye daraja.
Tyler Clementi, Mwanafunzi wa kiume wa mwaka wa kwanza wa chuo kikuu cha Rutgers University cha nchini Marekani mwenye umri wa miaka 18 ambaye alikuwa akifanya ushoga kwa siri, amejiua mwenyewe kwa kujirusha toka kwenye daraja baada ya video yake akiingiliwa kinyume cha maumbile na mwanaume mwingine kurushwa LIVE kwenye internet.

Clementi alijirusha wiki iliyopita toka kwenye daraja la George Washington na kuangukia kwenye mto mkubwa wa Hudson River, last week, maiti yake ilipatikana juzi kwenye mto huo.

Clementi alichukua uamuzi wa kujiua baada ya kugundua marafiki zake aliokuwa akikaa nao chumba kimoja walimrekodi kwa siri wakati akifanya mapenzi na mwanaume mwingine na VIDEO za tukio hilo zilirushwa LIVE kwenye internet kupitia Webcam.

"Kama angekuwa kitandani na mwanamke, haya yote yasingetokea", alisema mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho.

"Kama asingeanikwa LIVE kwenye internet, mambo yake ya ndani yasingeanikwa na leo tungekuwa naye hapa", aliongeza mwanafunzi huyo.

Wanafunzi wawili mmoja wa kiume Dhraun Ravi na mwingine wa kike Molly Wei, ambao wote wana umri wa miaka 18, wamefunguliwa mashtaka ya kuvunja haki za msingi za Clementi.

Mahakama iliambiwa kuwa webcam ilitumika kurusha LIVE tukio la Clementi akiingiliwa na mwanaume mwingine mnamo septemba 19 na Ravi alijaribu kulirusha LIVE tena tukio la pili lililofanyika septemba 21 ambayo ni siku moja kabla ya Clementi kujiua.

Taasisi za kutetea haki za mashoga zimeichachamalia kesi hii zikitaka Ravi na mwenzake wahukumiwe adhabu kali.

Taasisi hizo zimesema kuwa Ravi na mwenzake wameonyesha chuki waliyo nayo kwa mashoga na wasagaji na wameitaka mahakama itoe adhabu kali.

Ravi na mwenzake huenda wakahukumiwa kwenda jela miaka mitano iwapo watapatikana na hatia ya kuingilia undani wa mtu bila ya ridhaa yake.

source nfahamishe

Kahaba Ajitamba Kula Uroda na Beckham

Wednesday, September 29, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Kahaba Irma Nici ameendelea kujitamba kuwa alikula uroda na mcheza soka maarufu wa Uingereza, David Beckham ingawa Beckham anajiandaa kufungua kesi ya madai ya fidia kiasi cha dola milioni 16.
Pamoja na kwamba wanasheria wa mcheza soka maarufu wa Uingereza, David Beckham anayesakata kabumbu nchini Marekani wako kwenye jitihada za kufungua kesi mahakamani kumdai fidia ya dola milioni 16, kahaba anayedai kutembea na Beckham ameibuka na kutamba ana ushahidi wa kuthibitisha madai yake.

Kahaba Irma Nici mwenye asili ya Bosnia amedai kuwa anaweza kuithibitishia mahakama kuwa alilala na nyota huyo wa soka mjini London na mjini New York mnamo mwaka 2007.

Nici amedai kuwa Beckham ana alama za kipekee kwenye sehemu zake nyeti hivyo ajiandae kuvua suruali yake mahakamani ili kuzithibitisha alama hizo.

Nici mwenye umri wa miaka 26 amekuwa akiwakwepa wanasheria wa Beckham na amekuwa akijificha kwenye hoteli mjini New York.

Beckham mwenye umri wa miaka 35 anamshtaki Nici kutokana na habari iliyotoka kwenye jarida moja la Marekani kuwa Beckham alinunua penzi la kahaba Nici.

Nici aliliambia jarida hilo kuwa alishea kitanda kimoja na Beckham wakati Beckham alipofanya mapenzi yaliyowahusisha wanawake wawili kwa mpigo. Mwanamke wa pili aliyezungumziwa katika habari hiyo bado hajajulikana.

Beckham anamshtaki Nici na jarida hilo kwa kuandika habari za kumpakazia kuwa aliisaliti ndoa yake na Victoria Beckham, 36,

Beckham pia anamshtaki Nici na jarida hilo kwa habari ambayo imemfanya Beckham aonekane aliyatia maisha ya mkewe hatarini kwa kutembea na kahaba.

source nifahamishe

Sita Mbaroni Kwa Kuichoma Moto Quran Uingereza

Friday, September 24, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Polisi wa nchini Uingereza wamewatia mbaroni watu sita kwa kueneza chuki katika jamii kwa kuweka VIDEO kwenye YouTube wakionyesha jinsi wanavyoichoma moto Quran na kuipiga mateke.
Polisi wa nchini Uingereza wametoa taarifa wakisema kuwa wamewatia mbaroni watu 6 ambao waliweka video kwenye YouTube wakionyesha jinsi walivyoichoma moto misahafu na kuipiga mateke.

Taarifa ya polisi ilisema kuwa watu wawili walitiwa mbaroni septemba 15 na wengine wanne walitiwa mbaroni juzi jumatano. Wote wako nje kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea.

"Walikamatwa kufuatia tukio la kuchoma moto misahafu miwili katika kitongoji cha Gateshead siku ya septemba 11", alisema msemaji wa polisi.

"Tukio hilo lilirekodiwa na baadae kuwekwa kwenye internet", iliendelea kusema taarifa ya polisi.

Video hiyo ya YouTube iliwaonyesha wanaume walioficha sura zao kwa vitambaa wakipiga kelele za "Septemba 11, siku ya kimataifa ya kuichoma moto Quran" wakitukana na pia wakiimba "Hii ni kwaajili ya vijana wetu waliopo Afghanistan".

Wanaume hao walichukua mafuta ya petroli na kuyamwaga kwenye misahafu miwili na kuichoma moto misahafu hiyo.

Waliendelea kuimba na kupiga kelele wakati misahafu hiyo ikiendelea kuungua kabla ya kuanza kuipiga mateke.

Polisi kwa kushirikiana na uongozi wa kitongoji hicho ulitoa taarifa ya pamoja wakilaani kitendo hicho na kusema kuwa vitendo vilivyoonyeshwa kwenye video hiyo haviwakilishi mawazo ya jamii.

"Jamii yetu imeundwa kwa heshima kwa watu wote na tunaendelea kushirikiana na viongozi wa jumuiya, wakazi na watu wa imani zote ili kudumisha ushirikiano uliopo", ilisema taarifa hiyo.

Kutiwa mbaroni kwa wanaume hao kumekuja zikiwa hazijapita wiki mbili tangu mchngaji wa nchini Marekani, mchungaji Terry Jones alipoahirisha mpango wake wa kuichoma moto misahafu 200 katika kuadhimisha siku ya kuwakumbuka wahanga wa shambulizi la septemba 11, 2001.

source nifahamishe