Amuuza Binti Yake Ili Apate Pesa za Pombe

Wednesday, August 18, 2010 / Posted by ishak /


Mwanaume mmoja nchini India, anashikiliwa na polisi baada ya kumuuza binti yake mwenye umri wa miaka sita ili aweze kupata pesa za kununulia pombe.
Mwanaume huyo chapombe mwenye umri wa miaka 40 aliyetajwa kwa jina la Krishnaiah, alimuuza binti yake mwenye umri wa miaka sita ili aweze kupata pesa za kununulia pombe.

kwa mujibu wa gazeti la The Times la India, Krishnaiah alikuwa na kiu ya pombe kali lakini alipoenda kwenye duka la jirani ambalo hununua pombe siku zote, alitolewa nduki kwakuwa alikuwa akidaiwa pesa na mwenye duka.

Ili aweze kukata kiu yake ya pombe, Krishnaiah aliamua kumuuza binti yake mtaani kwa bei ya kuanzia rupia 300 ambazo ni sawa na Tsh. 8000.

Hatimaye alifanikiwa kumuuza binti yake kwa rupia 1,000 ( Tsh. 28,000).

Polisi walipewa taarifa na walifanikiwa kumuokoa binti huyo aliyeuzwa na baba yake kabla ya mnunuzi hajatoweka naye.

Katika tukio hilo lililotokea katika jimbo la Kadapa, Krishnaiah alikamatwa na kutupwa rumande.

Mnunuzi wa binti yake alifanikiwa kukimbia kabla hajatiwa mikononi mwa polisi

source nifahamishe