Ajaribu Kujiua Kwa Kukosa Matiti Makubwa

Wednesday, February 16, 2011 / Posted by ishak /

Mrembo wa Brazil ambaye awali alikuwa akishikilia rekodi ya dunia ya kuwa na matiti makubwa kuliko wanawake wote duniani na baadae matiti hayo kukatwa ili kuokoa maisha yake, amejaribu kujiua kwa mara ya pili akisema kuwa hawezi kuishi bila ya matiti
Mrembo Sheyla Hershey wa nchini Brazil ambaye mwaka jana matiti yake makubwa yalikatwa ili kunusuru maisha yake alipopatwa na maambukizi kwenye matiti yake, amejaribu kujiua kwa mara ya pili.

Sheyla alifanya operesheni nyingi za kuongeza matiti yake ili kuvunja rekodi ya kuwa na matiti makubwa kuliko wanawake wote duniani. Alifanikiwa kuvunja rekodi hiyo lakini aliipoteza rekodi hiyo mwaka jana baada ya madaktari kuamua kuyakata matiti yake ili kuyaokoa maisha yake yalipokuwa hatarini kutokana na maambukizi.

Kutokana na kushindwa kuishikilia rekodi ya dunia ya matiti makubwa, mwezi uliopita Sheyla alijaribu kujiua kwa mara ya kwanza akisema kuwa hawezi kuishi bila ya matiti yake makubwa.

"Bila ya matiti yangu makubwa nachukiza na nakuwa sijielewi", alisema Sheyla ambaye anaishi Texas nchini Marekani.

Sheyla alishawahi kupatiwa matibabu ya kisaikolojia kutokana na lindi la mawazo la kupoteza kitambulisho chake cha mwanamke mwenye matiti makubwa kuliko wote duniani.

Jumapili wiki iliyopita, Sheyla alijaribu kujiua kwa mara ya pili kwa kumeza kiasi kikubwa cha vidonge.

Sheyla ambaye ana umri wa miaka 31 bado amelazwa hospitali tangu jumapili akiwa kwenye chumba cha watu mahututi.

"Madaktari hawajui ni wakati gani atazinduka, tunamuombea dua aweze kuzinduka", alisema mumewe.


source nifahamishe