Kuna mambo kadhaa yanayoweza kusababisha unene uliopitiliza. Mambo hayo ni pamoja na
- Vyakula vya mafuta – Ulaji wa vyakula venye mafuta mengi au calories nyingi.
- Kutofanya mazoezi – Wale wasiofanya mazoezi mara kwa mara huwa wanene tofauti na wale wanaofanya mazoezi.
- Kurithi viashiria vya asili (genes) – Viashiria hivi vinaweza kuwa moja ya vichocheo vya kuongeza uzito kwani ndivyo huamua wapi mafuta huhifadhiwa mwilini na kwa kiwango gani. Lakini haimanishi kuwa mtu akiwa navyo basi ndio atakumbwa na tatizo hili.
- Umri – Watu wengi huongezeka uzito au hunenepa kadri umri unavyoongezeka kwa sababu wanakuwa hawajishughulishi sana (less active) na huwa wanapungua maumbile ya miili yao (muscles mass)
- Matatizo ya kisaikolojia – Wakati mwengine watu wenye matatizo ya kisaikolojia au msongo wa mawazo (stress) huwa na tabia ya kula sana, matokeo yake ni kunenepa.
- Dawa – Baadhi ya dawa zenye madhara ya kuongeza unene ni kama corticosteroids, blood pressure medications, tricyclic medications na kadhalika.
- Matatizo ya afya – Baadhi ya magonjwa yanachangia kuongezeka kwa uzito au kenenepa kama cushings syndrome, hypothyroidism, osteoarthritis na kadhalika
Vihatarishi vya tatizo la unene wa kupitiliza
Aidha yapo mambo kadhaa ambayo yanaweza kumuhatarisha mtu kupata unene wa kupitiliza. Mambo haya ni pamoja na
- Kukua kwa uchumi wa nchi – Wananchi wengi wanaoishi kwenye nchi zilizoendelea au wenye kipato kikubwa ndio wanaopata tatizo hili kutokana na kuishi mfumo wa maisha ya kivivu na hali ya kutokufanya mazoezi (sedentary lifestyle).
- Historia ya kuongezeka uzito uliopitiliza kwenye familia nayo yaweza kuhatarisha mtu kupata tatizo hili. Aidha, si jambo la kushangaza kuona karibu familia nzima au wengi wa wanafamilia kuwa wanene kupitiliza.
- Kutojishughulisha na chochote (inactive).
- Kupenda kula sana kuliko kawaida (overeating).
- Kula vyakula vya mafuta mengi
- Kutumia dawa zenye madhara ya kuongeza uzito uliopitiliza.
- Kuwa na ugonjwa wa vichocheo mwilini (hormonal disorders) kama cushingsyndrome, hypothyroidism.
- Kuwa na msongo wa mawazo au kuathirika kisaikolojia.
Magonjwa yanaoweza kuambatana na tatizo la unene uliopitiliza
- Kisukari
- Shinikizo la damu (hypertension)
- Kiharusi (Stroke)
- Magonjwa ya moyo
- Tatizo la kutopumua vizuri wakati mtu yupo usingizini (Sleep apnea)
- Vijiwe katika mfuko wa nyongo (Gallstones)
- Kiwango cha juu cha lijamu kwenye damu (cholesterol ikiwemo triglycerides)
- Ugonjwa wa mifupa kama yabisi (osteoarthritis).
- Saratani ya matiti
- Saratani ya tezi dume (prostate cancer)
- Saratani ya utumbo mpana pamoja na maeneo ya haja kubwa (Colorectal cancer)
- Matatizo ya mzunguko na mishipa ya damu kama vile kuvimba kwa vena za miguuni(varicose veins)
Tiba ya kuongezeka unene kupita kiasi
Tiba ya tatizo hili ni mhusika kujitambua ya kwamba ana tatizo na kuwa tayari kupunguza uzito. Mabadiliko ya tabia ya mhusika ni muhimu sana, mabidiliko haya yawe ndio mfumo wa maisha yake ya kila siku.
Kupungua uzito na kujilinda au kutunza uzito ulionao baada ya kupunguza uzito ni jambo la msingi sana na inahusisha mazoezi, chakula na madiliko ya tabia ya mtu.
- Mabadiliko ya tabia - Hii inahusisha muhusika kupunguza kiwango cha chakula anachokula lakini kiwe chenye virutubisho vyote muhimu vya afya na kuongeza kiwango cha ufanyaji mazoezi.
- Mazoezi - Mazoezi husaidia kupunguza uzito hasa kipindi cha miezi sita ya mwanzo na hutunza uzito uliokusudiwa kwa muda mrefu. Pia hupunguza mafuta ya mwilini, huongeza ufanisi wa moyo, hupunguza tatizo la shinikizo la damu (hypertension), na kuweka sukari katika kiwango kinachohitajika mwilini.
Kama hujazoea kufanya mazoezi ni vizuri uanze taratibu na ujiwekee lengo kwa kufanya mazoezi kwa muda wa nusu saa kila siku, siku tano kwa wiki,(dakika 30 kila siku kwa siku tano kwa wiki). Mazoezi mazuri ni kama kuogelea, kuendesha baiskeli, kutembea, kunyanyua vitu vizito (visiwe vyenye uzito mkubwa), mazoezi ya viungo na kadhalika. Kama mtu ni mnene sana basi ni bora kuzungumza na daktari wako kabla ya kuanza mazoezi mapya. Baada ya kuanza mazoezi kwa mara ya kwanza, mwili utakuwa na maumivu, hii ni kawaida lakini kama mtu atapata maumivu zaidi ya masaa 2 baada ya kufanya mazoezi ni vizuri kumuona daktari.
- Dawa - Zipo dawa nyingi za kupunguza uzito lakini ikumbukwe ya kwamba hakuna tiba ya tatizo hili na dawa hizi zina madhara mengi kama kuongeza shinikizo la damu (hypertension), matatizo ya moyo, kuharisha,msongo wa mawazo (depression) na mengineyo.
- Chakula - Msingi wa kupunguza uzito au unene ni kujua ni kiwango gani cha caloriesmwili wako unahitaji kwa siku ili uwe unakula chakula ambacho hakitazidisha au kupunguza kiwango cha calories unazohitaji kwa siku. Mlo mzuri ni ule ulio na matunda kwa wingi, mboga za majani, nafaka ambazo hazijakobolewa, mafuta kidogo (less saturated fat). Vyakula vengine ni kama mayai, nyama isiokuwa ya mafuta (lean meat), samaki, kuku na vingineyo.
- Tiba ya upasuaji - Kuna aina nyingi za upasuaji ambao unasaidia kupunguza uzito aina hizi ni kama gastric banding, gastric bypass (Roux-en-Y-procedure), liposuction. Kabla ya kufanyiwa upasuaji, muhusika atahitaji kupimwa kisaikolojia (psychological testing) na kupewa ushauri nasaha kwani tiba hii pia ina madhara yake.
Wanawake ambao wana uzito wa kupitiliza (obese women) wakiwa wajawazito wako kwenye hatari ya kupata madhara yafuatayo;
- Kisukari cha mimba (Gestatitional diabetes) – kisukari hiki kinatokea wakati wa ujauzito na hupotea baada ya kujifungua mtoto.
- Shinikizo la damu (hypertension)
- Shinikizo la damu wakati wa ujauzito pamoja na kifafa cha mimba (pre-eclampsia & eclampsia)
- Kuzaa kwa njia ya upasuaji (caesarean section)
- Tatizo la kiumbe kutopata hewa vizuri wakati wa ujauzito (fetal distress)
0 comments:
Post a Comment