Mapenzi Yamzingua Bibi wa Miaka 92, Ampiga Mtu Risasi

Thursday, March 24, 2011 / Posted by ishak /Bibi Helen Staudinger

Bibi mwenye umri wa miaka 92 wa nchini Marekani ametiwa mbaroni kwa kumpiga risasi mwanaume jirani yake ambaye alikataa kumpa 'denda' bibi huyo ambaye alizidiwa na penzi kwa jirani yake ambaye siku zote alikuwa akimtolea nje bibi huyo.
Bibi Helen Staudinger mjane mwenye umri wa miaka 92 mkazi wa Florida nchini Marekani ametiwa mbaroni kwa kuishambulia kwa risasi nyumba ya jirani yake ambaye alikataa kumpa busu.

Helen aliwaambia polisi kuwa alienda kwa jirani yake mwenye umri wa miaka 53, Dwight Bettner, na kumuomba ampe angalau busu ili autulize moyo wake uliojaa cheche za mapenzi kwa jirani huyo.

Baada ya Dwight kukataa kumbusu Helen, Helen alisema kuwa hataondoka mlangoni kwake hadi pale Dwight atakapokubali kumbusu.

Helen aliwaambia polisi kuwa mzozo mkubwa ulizuka kati yake na Dwight na kupelekea bibi huyo arudi nyumbani kwake kuchukua bunduki na kuanza kuishambulia kwa risasi nyumba ya Dwight.

Mojawapo ya risasi ilipenya kwenye dirisha la chumba cha Dwight na kusababisha Dwight kujeruhiwa na vioo va dirisha hilo. Risasi zingine tatu zilipigwa kwenye kuta za nyumba ya Dwight.

Dwight aliliambia gazeti la Star-Banner kuwa kwa miezi sita tangu alipohamia nyumba ya jirani na bibi Helen, amekuwa akisumbuliwa na bibi huyo anayemtaka kimapenzi.

"Nilimwambia kuwa nina uhusiano na mwanamke mwingine lakini alikuwa akisisitiza lazima niwe mpenzi wake", alisema Dwight.

Dwight aliongeza kuwa bibi Helen aliwahi kumshambulia mwanamke mmoja ambaye alifikiria alikuwa ndiye mpenzi wa Dwight.

Bibi Helen amefunguliwa mashtaka ya kufanya shambulizi la silaha kwenye makazi ya watu.


source nifahamishe