Mke wa Rais Adai Talaka

Thursday, March 24, 2011 / Posted by ishak /


Sandra Torres de Colom
Mke wa rais wa Guatemala ameamua kuivunja ndoa yake ya miaka minane ili aweze kugombea urais.
Mahakama ya nchini Guatemala imeanza kusikiliza kesi ya mke wa rais wa Guatemala ambaye ameenda mahakamani kudai talaka ili kuivunja ndoa yake ya miaka minane na rais Alvaro Colom.

Mke huyo wa rais, Sandra Torres de Colom ameamua kuivunja ndoa yake ili aweze kuwania kiti cha urais ambacho mume wake atakiachia atakapomaliza muda wake mwezi septemba mwaka huu. Mume wake anamaliza miongo yake miwili ya uongozi na hataruhusiwa kugombea tena urais.

Sheria za Guatemala zinakataza watu wa familia ya rais kushiriki kwenye uchaguzi wa kugombea urais.

Sandra alitangaza wiki iliyopita kuwa atagombea urais mwaka huu kwa kupitia chama tawala National Unity for Hope party.

Kama rais Colom atakubali kutoa talaka kuivunja ndoa yake basi Sandra ataruhusiwa kisheria kugombea urais.

source nifahamishe