Mbunge Anayepiga Vita Sinema za Ngono Anaswa Akiangalia Ngono Bungeni

Saturday, April 16, 2011 / Posted by ishak /


Arifinto akipiga chabo video za ngono ndani ya Bunge

Mbunge wa nchini Indonesia ambaye alijipatia umaarufu kwa kusimama kidete kushinikiza sheria kali zipitishwe kama vile kutupwa jela miaka 15 kwa kushiriki kwenye video za ngono, mbunge huyo amelazimika kujiuzulu baada ya kunaswa akiangalia ngono bungeni.
Arifinto, mwanasiasa wa nchini Indonesia ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kupigania sheria za kupinga video na picha za ngono, amenaswa akiangalia video ya ngono ndani ya kikao cha bunge.

Arifinto alilazimika kujiuzulu ubunge baada ya picha zake kusambaa kwenye vyombo vya habari zikimwonyesha akiwa bize kwenye laptop yake akiangalia video ya ngono.

Arifinto alikuwa miongoni mwa wanasiasa walioshinikiza na hatimaye kupitishwa kwa sheria ya kupinga picha, video na vitendo vya ngono hadharani.

Sheria hiyo iliyopitishwa mwaka 2008 inaweka wazi kuwa adhabu ya kutupwa jela hadi miaka 15 au kupigwa faini itamkumba mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kubusiana hadharani au kuangalia picha au video za ngono.

Kuzionyesha, kuzimiliki au kuzihifadhi video au picha za ngono ni marufuku kwa mujibu wa sheria hiyo.

Arifinto mwenye umri wa miaka 51 ambaye pia ni baba wa watoto watano, alikuwa ndio msemaji mkubwa wa kushinikiza kupitishwa kwa sheria hiyo.

Arifinto aliitisha kikao na kutangaza mbele ya waandishi wa habari kuwa anajiuzulu ubunge wake mara moja.

"Huu ni uamuzi wangu, hakuna mtu aliyenishinikiza kufanya hivyo", alisema Arifinto ambaye kama raia wengine wa Indonesia anajulikana kwa jina moja tu.

Indonesia, ni nchi ya kidemokrasia yenye jumla ya watu milioni 237, ndiyo nchi yenye waislamu wengi kuliko nchi zote duniani.


source nifahamishe