Shakira Aingizwa Mjini na Kibaka

Saturday, April 16, 2011 / Posted by ishak /


Shakira

Mwanamuziki maarufu duniani wa muziki wa Pop, Shakira ambaye anajulikana sana kwa kunyonga kiuno chake, ameibiwa pete yake ya thamani wakati alipokuwa akiwasalimia kwa kuwapa mkono washabiki wake waliohudhuria shoo yake nchini Mexico.
Shakira mwenye umri wa miaka 34, alikuwa akipafomu kwenye shoo yake katika chuo kikuu cha University of Monterrey kilichoko kwenye mji wa Monterrey, Mexico siku ya alhamisi wakati kibaka mmoja alipofanikiwa kuivua pete ya nyota huyo wa muziki wa Pop.

Shakira ambaye alikuwa akiwasalimia kwa kuwapa mkono washabiki wake, aligundua muda mfupi baadae kuwa pete yake ameishavuliwa.

Tukio hilo la wizi lilinaswa live na mpiga picha za video katika shoo hiyo hata hivyo Shakira hakukatisha shoo yake na wala hakumkamata mwizi wake.

Hakuna mtu aliyekamatwa hadi sasa kutokana na tukio hilo.

Wakati huo huo, mpenzi wa Shakira, nyota wa soka beki wa timu ya Barcelona ya Hispania, Gerard Pique amesema kuwa ingawa anafurahia kuwa kwenye mahusiano na Shakira lakini bado hajazoea maisha ya kufuatiliwa kila kona na paparazzi ambao wamekuwa wakimfuatilia nyota huyo wa soka tangu ilipojulikana kuwa anatoka na Shakira.

"Huwa wanakuja kundi kubwa, inabidi kuzoea hali hii ya kufuatwa mitaani kila kona", alisema Pique.


source nifahamishe