Vurugu zatanda vituo vya mafuta

Wednesday, August 10, 2011 / Posted by ishak /

NewsImages/5866906.jpg

VURUGU, FUJO za hapa na pale zilitawala jana katika vituo mbalimbali viuzavyo mafuta jijini Dar es salaam kutokana na baadhi ya vituo kugoma kuuza mafuta hali iliyofanya kuleta adha kwa watumiaji wa vyombo vya moto
Msongamano mkubwa wa watu waliobeba vidumu mikononi na foleni ya ndefu ya magari vilitawala katika vituo hivyo kusaka nishati hiyo ambapo ilikuwa adimu kupatikana.

Msongamano huo ulioanza mapema jana ulizua tafrani baada ya watu kuanza kugombea huduma hiyo huku kila mmoja akiwa na hofu ya kukosa huduma hiyo.
Hali hiyo imekuja baada ya baadhi ya vituo juzi na jana kugoma kuuza mafuta ya petrol kutokana na Serikali kuamrisha vituo hivyo kuuza bei elekezi iliyopangwa hali iliyofanya kuwa na upungufu wa upatikanaji wa mafuta kama awali.

Vituo vya Bigbon, Lake Oil ndivyo vilionekana kutoa huduma hiyo na watu wengi kukimbilia huko hali iliyofanya mmiliki kuuza mafuta yasiyozidi ya shilingi elfu kumi ili kila mmoja aweze kupata huduma hiyo.

Hali ilikuwa mbaya katika kituo cha Bigbon kilichopo Msimbazi ambapo madereva wa magari na pikipiki kugombania huduma hiyo huku kituo cha Sinza wakigoma kuzia watu wenye vidumu kwa hofu ya kudhani wanakwenda kufanya biashara

Hali hiyo iliwafanya wachanganyikiwe kwa kuwa kuna baadhi ya magari yalizimika njiani na kushindwa kufika kituoni na kufanya fujo kutanda na wengine kutaka kutoa adhabu kwa muuzaji wa mafuta

Serikali ilitangaza mafuta ya petrol yauzwe kwa bei ya Shilingi 2004 na dizeli iuzwe kwa Shilingi1911ambapo wenye vituo walionyehsa kuwatunishia misuli serikali huku serikali nayo kutoa onyo kiuwafutia leseni wale wote wagomao kutoa huduma hiyo

Uchunguzi wa NIFAHAMISHe umebaini jana baadhi ya watu waliuziwa mafuta kwa bei ya zaidi ya shilingi elfutano kutokana na adha hiyo

source nifahamishe