Achaniwa nguo na wapiga debe

Friday, March 05, 2010 / Posted by ishak / comments (0)

MSICHANA mmoja jina lake halikuweza kupatikana maramoja alijikuta yupo kwenye wakati mgumu baada ya kuchaniwa nguo yake aliyovaa na wahuni na kumuacha na aibu kedekede na akiwa hana la kufanya kwa wakati huo.
Tukio hilo la aibu lilitokea jana majira ya saa 2 usiku, maeneo ya Magomeni Kagera wakati msichana huyo akiwa kituoni hapo akisubiri usafiri.

Wahuni hao walianza kumshambulia kwea maneno dada huyo na msichana huyo kuwajibu jeuri na hivyo wahuni hao waliamua kumchania nguo yake ya isiyo na heshima aliyoivaa.

Msichana huyo alivaa nguo fupi kupita kiasi, alivaa blauzi tu na kuigeuza gauni hivyo kupelekea maungo yake ya mwili kuonekana ambapo wahuni hao waliamua kumfanyia uhuni kumchania ng uo hiyo ili atembee kama alivyozaliwa kabisa.

Wahuni hao walimshika dada huyo na kumchania gauni hilo na kupiga kelele na hakuna hata msamaria mwema mmoja aliyeweza kumsaidia wka wakati huo kwa kuwa hakuna mtu aliyependezwa na uvaaaji wake huo.

Wahuni hao ambao walikuwa zaidi ya wawili walishirikiana kwa pamoja kumshikisha adabu dada huyo na kumuacha akilia kituoni hapo na nguo yake kuichana.

“Tumeanza na wewe leo, na wengine watafuata tunataka mpate adabu si mteembee uchi tu” walisikika wakaka hao

source nifahamishe

Wengine watano wauawa Mara

Friday, March 05, 2010 / Posted by ishak / comments (0)

WATU WENGINE watano wameuwa na wengine zaidi ya kumi kujeruhiwa usiku wa kuamkia leo huko Tarime Mkoani Mara.
Watu hao wameuawa usiku wa kuamkia leo kwa kukatwakatwa na mapanga na kupelekea vifo vyao wakati wakiwa katika kusherehekea harusi.

Kamanda wa Polisi Mara, Bw. Constantine amesema kuwa watu hao walikuwa katika harusi kwa mzee Mwita Burure na mauti hayo yaliwakuata hapo.

Amesema kuwa walizuka watu ambao hawakufahamika mara moja waliwavamia katika harusi hiyo na kuua watu na kujeruhi wengine zaidi ya kumi.

Amesema maiti hizo zimehifadhiwa na majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya Mkoa kwa matibabu zaidi.

Amsema ucbhunguzi zaidi juu ya tukio hilo linafanyika na kuwakamata waliohusika na tukio hilo la kinyama.

Tukio hili ni la tatu katika wiki mbili hizi mfululizo ambapo inadaiwa ni visasi vinavyolipizwa katika koo mkoani humo kwa kuli[izana kutokana na mauaji ya kinyama yaliyotokea mwezi ulipita kwa kuuawa watu 17 wa familia moja.


source nifahamishe

Kondomu Ndogo Kwaajili ya Watoto Zaingia Madukani

Friday, March 05, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Kampuni kubwa ya kutengeneza kondomu ya Uswizi imetengeneza kondomu ndogo sana kwaajili ya watoto kuanzia umri wa miaka 12 kutokana na kile kinachosemwa kuwa watoto wa siku hizi wanaanza kufanya ngono mapema.
Kondomu hizo zilizopewa jina la "Hotshot" ni maalumu kwa vijana wa kiume wenye umri mdogo kuanzia umri wa miaka 12 hadi miaka 14.

Kondomu hizo zilitengenezwa kufuatia hatua ya makundi ya uzazi wa mpango kusema kuwa vijana wenye umri mdogo hawapati kinga inayotakikana wakati wa kujamiiana.

Ilidaiwa kuwa vijana wa siku hizi wanaanza ngono mapema na hawatumii kinga na wala hawajui jinsi ya kujikinga na magonjwa yanayotokana na ufanyaji wa ngono zisizo salama.

Kondomu hizo zimeingia madukani nchini Uswizi na kuzua maoni tofauti toka kwa wazazi nchini Uswizi.

Taarifa ya utafiti uliofanyika kabla ya kutengenezwa kwa kondomu hizo ilionyesha kuhitajika kwa elimu ya mapema kwa vijana jinsi ya kujikinga na magonjwa ya zinaa pamoja na mimba zisizohitajika.

Msemaji wa kampuni ya Lamprecht AG iliyotengeneza kondomu hizo, alisema kuwa watakapoanza kuuza kondomu hizo nje ya nchi, Uingereza itapewa nafasi kubwa kutokana na idadi kubwa ya mimba za wasichana wenye umri mdogo.

Katika nchi za ulaya Uingereza inaoongoza kwa idadi kubwa ya wasichana wanaopata ujauzito kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.

source nifahamishe

Rihanna Amwaga Radhi Kwenye Bethidei Yake

Friday, March 05, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Nyota wa muziki wa Marekani Rihanna alisherehekea kutimiza miaka 22 kwa shoo toka kwa mwanamke mcheza ngono ambaye ni mfupi kuliko wanawake wote wanaoshiriki kwenye sinema za ngono.
Rihanna alisherehekea kutimiza miaka 22 kwa sherehe ya "Suprise" iliyoandaliwa na mpenzi wake nyota wa mchezo wa baseball, Matt Kemp.

Katika sherehe hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi mmoja mjini Phoenix, Arizona, shoo maalumu ya dansi la kupagawisha watu ilitolewa na mcheza video za ngono mfupi kuliko wote duniani "Midget" mwenye urefu wa mita 1.1 ambaye ana umri wa miaka 29.

Katika sherehe hiyo Rihanna akiwa amevalia kivazi cha kudatisha alinyanyuka na kujitosa ukumbini na kupagawisha watu kwa mauno yake.

Keki ya Bethidei ya Rihanna ilikuwa katika umbile la maboksi ya viatu katika kukumbushia jinsi Rihanna anavyopenda kununua na kuvaa viatu vya wanamitindo mbali mbali.

source nifahamishe

Madhara ya Mabomu ya Marekani, Watoto wa Ajabu Wazaliwa Iraq

Friday, March 05, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Madhara ya mabomu ya Marekani nchini Iraq yanajidhirisha kwa idadi kubwa ya watoto wenye vilema na maumbile ya ajabu ajabu kama vile watoto wenye vichwa vitatu kuzaliwa nchini Iraq na kuwafanya maafisa wa Iraq wawashauri wanawake wafunge kizazi.
Marekani inahisiwa kuwa ilitumia mabomu ya kikemikali katika mashambulizi yake ya mabomu nchini Iraq mwaka 2004, hii inatokana na idadi kubwa sana ya watoto wanaozaliwa wakiwa na maumbile ya ajabu ajabu.

Katika mji wa Fallujah ambapo ndipo mabomu mengi ya Marekani yalidondoshwa kuung'oa upinzani wa majeshi ya Saddam, idadi kubwa sana ya watoto wenye matatizo mbali mbali wamekuwa wakizaliwa kiasi cha kuwafanya madaktari wawashauri wanawake wa Fallujah wasizae.

Baadhi ya watoto wamekuwa wakizaliwa wakiwa na matatizo ya akili, wengine matatizo ya moyo huku wengine wakiwa na maumbile yasiyo ya kawaida.

Mwandishi wa BBC, John Simpson, aliyetoa ripoti yake toka Fallujah alikiri kushuhudia idadi kubwa ya watoto wenye maumbile ya ajabu.

Mmoja wa watoto hao alikuwa na vichwa vitatu wakati mwingine alikuwa na jicho moja huku watoto wengi wakiwa na maumbile ya kutisha zaidi.

Idadi ya watoto wanaozaliwa wakiwa na matatizo ya moyo, ubongo au kupooza upande mmoja ni wengi sana kiasi cha kwamba madaktari wanasema kuwa kila siku watoto watatu wanazaliwa mjini Fallujah wakiwa na kasoro kwenye maumbile yao.

Maafisa wa Iraq wanawashauri wanawake wa Fallujah kuziacha ndoto zao za kuwa na watoto kwani watoto watakaozaliwa watakuwa na maumbile ya ajabu.

Majeshi ya Marekani yaliumiminia mabomu makubwa mji wa Fallujah kiasi cha kwamba nusu ya nyumba zote za Fallujah na misikiti ilibomolewa.

Marekani ilikiri kutumia mabomu hatari ya phosphorus ambayo yamepigwa marufuku duniani kutumika kwenye vita kutokana na uharibifu mkubwa unaotokana na mabomu hayo.

Majeshi ya Marekani yalianza mashambulizi yake mjini Fallujah kuanzia novemba 7 mwaka 2004 na baada ya siku 9 walitangaza kuuteka mji huo.

Wanajeshi 51 wa Marekani walifariki kwenye mashambulizi hayo wakati wanamgambo wa Iraq 1,400 waliuliwa kwenye mashambulizi hayo.

source nifahamishe

Rubani Mwenye Vyeti Feki Aendesha Ndege Kwa Miaka 13

Friday, March 05, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Maafisa wa Uholanzi wamemkamata rubani feki raia wa Sweden ambaye kwa kutumia vyeti feki vya urubani amekuwa akiendesha ndege za abiria kwa miaka 13 bila kugundulika.
Rubani huyo mwenye umri wa miaka 41 alitiwa mbaroni kwenye uwanja wa ndege wa Schiphol mjini Amsterdam akijiandaa kuirusha ndege ya abiria 101 toka Uholanzi kuelekea Uturuki.

Rubani huyo mwenye makazi yake mjini Milan nchini Italia kwa miaka 13 alitumia vyeti feki na kufanikiwa kuendesha ndege za abiria za mashirika ya ndege ya Uingereza, Italia na Ubelgiji.

Kufuatia taarifa waliyotonywa na maafisa wa Sweden, maafisa wa Uholanzi walimnyanyua rubani huyo toka kwenye kiti cha rubani wakati akijiandaa kuanza safari ya kuelekea Uturuki akiwa na abiria 101 kwenye ndege aina ya Boeing 737.

Taarifa zilisema kuwa rubani huyo aliwahi kuwa na leseni ya kuendesha ndege ndogo ambayo pia ilikuwa imeisha muda wake na alikuwa haruhusiwi kuendesha ndege kubwa.

Wakati anakamatwa rubani huyo ambaye jina lake liliwekwa kapuni alikuwa akiendesha ndege ya shirika la Uturuki la Corendon Airlines.

Rubani huyo amewekwa mahabusu mjini Amsterdam akisubiria kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kufoji vyeti na kuendesha ndege bila leseni.

source nifahamishe

Mugabe Kugombea Urais Kwa Mara Nyingine

Friday, March 05, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 86 amesema yuko tayari kugombea urais kwa mara nyingine kuliongoza taifa la Zimbabwe.
Akiongea na waandishi wa habari mjini Harare, rais Robert Mugabe ambaye anaendelea kuiongoza Zimbabwe kwa miaka 30 sasa, alisema kuwa yuko tayari kugombea tena urais kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika miaka miwili ijayo.

Mugabe alisema kuwa iwapo chama chake cha ZANU-PF kitampitisha kugombea urais basi atasimama kwa mara nyingine kugombea urais.

Mugabe ambaye alianza kuitawala Zimbabwe tangia ilipopewa uhuru wake kutoka kwa Waingereza mwaka 1980, alishinda uchaguzi wa urais uliopita ingawa kambi ya upinzani iligoma kukubali matokeo ya uchaguzi ikisema kuwa hila zilifanyika.

Hali hiyo ilisababisha mtafaruku nchini Zimbabwe ambapo uchumi wake uliyumba kutokana na vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na mataifa ya magharibi.

Pesa ya Zimbabwe ilipoteza thamani yake na kuifanya Zimbabwe izitose pesa zake na kuanza kutumia dola za kimarekani na Rand za Afrika Kusini kama mbadala wa pesa zake.

source nifahamishe