Wengine watano wauawa Mara

Friday, March 05, 2010 / Posted by ishak /

WATU WENGINE watano wameuwa na wengine zaidi ya kumi kujeruhiwa usiku wa kuamkia leo huko Tarime Mkoani Mara.
Watu hao wameuawa usiku wa kuamkia leo kwa kukatwakatwa na mapanga na kupelekea vifo vyao wakati wakiwa katika kusherehekea harusi.

Kamanda wa Polisi Mara, Bw. Constantine amesema kuwa watu hao walikuwa katika harusi kwa mzee Mwita Burure na mauti hayo yaliwakuata hapo.

Amesema kuwa walizuka watu ambao hawakufahamika mara moja waliwavamia katika harusi hiyo na kuua watu na kujeruhi wengine zaidi ya kumi.

Amesema maiti hizo zimehifadhiwa na majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya Mkoa kwa matibabu zaidi.

Amsema ucbhunguzi zaidi juu ya tukio hilo linafanyika na kuwakamata waliohusika na tukio hilo la kinyama.

Tukio hili ni la tatu katika wiki mbili hizi mfululizo ambapo inadaiwa ni visasi vinavyolipizwa katika koo mkoani humo kwa kuli[izana kutokana na mauaji ya kinyama yaliyotokea mwezi ulipita kwa kuuawa watu 17 wa familia moja.


source nifahamishe