Auliwa na Mumewe Akisherehekea Kupewa Talaka

Tuesday, December 01, 2009 / Posted by ishak /


Mama wa watoto wawili wa nchini Uingereza ameuliwa na mumewe baada ya kuandaa sherehe ya kusherehekea kupewa talaka.
Katrina Jones mwenye umri wa miaka 34 aliuwa na mumewe kwa kuchomwa chomwa na kisu masaa machache kabla ya kuanza kwa sherehe aliyoiandaa kusherehekea kupewa talaka.

Mwili wa Katrina ulikutwa ukiwa katika dimbwi la damu ukiwa na majeraha kibao ya kuchomwa na kisu asubuhi ya siku ya jumamosi masaa machache kabla ya wageni waalikwa kuanza kuwasili kwenye sherehe aliyoiandaa "Divorce Party" kusherehea kuvunjika kwa ndoa yake na mumewe.

Mume wake aliyejulikana kwa jina la Brian Jones mwenye umri wa miaka 63 alikamatwa na kushikiliwa na polisi na baadae kufunguliwa mashtaka ya mauaji.

Majirani zake walisema kuwa ndoa ya miaka 9 ya Katrina na Brian ilivunjika mwezi februari mwaka huu.

Siku ya ijumaa Katrina aliweka mabango kwenye madirisha ya nyumba yake katika kitongoji cha Marske, Middlesbrough akiwaalika watu katika sherehe yake ya kuvunjika kwa ndoa yake.

Lakini aliuliwa na mumewe siku iliyofuatia kabla hata ya kuanza kwa sherehe hiyo.

Majirani walimuelezea Brian kuwa ni mtu mwenye vurugu kiasi cha kuogopwa na majirani zake.

Majirani walisema kuwa Katrina aliamua kuachana na mumewe baada ya mapenzi yake kwa mumewe kuisha kutokana na tabia zake.

"Ilikuwa ni vigumu kwake kukubali kuwa ndoa yake na Katrina imevunjika", alisema mmoja wa majirani zake akielezea sababu iliyopelekea Brian kumuua mkewe.

Katrina alikuwa ni mke wa tatu wa Brian baada ya ndoa zake mbili za mwanzo kuvunjika.


source.nifahamishe.com

0 comments:

Post a Comment