Mapenzi! Mapenzi! Aifukua Maiti ya Mkewe na Kulala Nayo

Tuesday, December 01, 2009 / Posted by ishak /

Mwanaume mmoja wa nchini Vietnam ambaye alikuwa na huzuni ya kuondokewa na mkewe, alifukua kaburi la mkewe na kuichukua maiti ya mkewe na kuanza kulala nayo kitanda kimoja kwa kipindi cha miaka mitano.
Le Van aligubikwa na huzuni kubwa wakati mkewe alipofariki mwaka 2003 kiasi cha kwamba alianza kulala juu ya kaburi lake katika mji wa Quang Nam uliopo ukanda wa kati wa Vietnam.

Gazeti la Vietnamnet liliripoti kuwa Van aliendelea kulala juu ya kaburi la mkewe usiku kwa kipindi cha miezi 20 mpaka alipoanza kuugua kutokana na hali ya hewa ya baridi.

Ili kujikinga na baridi, Van aliamua kutengeneza handaki lililoenda kwenye jeneza lake na kuanza kulala pembeni ya maiti yake.

Watoto wa Van waliligundua handaki hilo na waliamua kumzuia Van kulitembelea kaburi la mkewe.

Mwezi novemba mwaka 2004, Van alilifukua kaburi la mkewe na kuichukua maiti ya mkewe hadi nyumbani kwake.

Van alitumia udongo mfinyazi kuizunguka mifupa ya maiti ya mkewe na kisha aliivalisha maiti hiyo nguo za kike na kisha kuipaka vipodozi.

Van mwenye umri wa miaka 55, baba wa watoto saba, alianza kulala pembeni ya maiti ya mkewe akiikumbatia kuanzia wakati huo hadi leo.

Picha zinazomuonesha Van akiwa pembeni ya maiti ya mkewe zilichapishwa kwenye gazeti la Vietnamnet, ikiwemo picha moja ambayo iliionyesha mifupa ya mkono wa mkewe ikiwa imezungushiwa udongo.

"Mimi ni mtu ninayependa kufanya vitu tofauti.. mimi si mtu wa kawaida", Van alisikika akiliambia gazeti hilo.


source.nifahamishe.com

0 comments:

Post a Comment