Mmasai Ang'oa Toto la Kizungu, Wazazi Wamtenga

Sunday, April 04, 2010 / Posted by ishak /


Binti wa Kiingereza ambaye kutokana na utajiri mkubwa wa baba yake, alizoea maisha ya kifahari akisafiri nchi mbalimbali duniani, ameangukia kwenye penzi la kijana wa kimasai nchini Kenya na kuamua kuolewa naye na kusababisha wazazi wake waamue kumtenga kupinga uamuzi wake huo.
Binti wa Kiingereza Colette Armand mwenye umri wa miaka 24 alizoea kuishi maisha ya kifahari akisafiri nchi mbali mbali na kukaa kwenye hoteli za kifahari.

Hata siku moja hakuwahi kufikiria kwamba siku moja angeangukia kwenye penzi la kijana wa kimasai anayeishi porini ambako hakuna umeme wala maji.

Baba yake Colette ni mfanyabiashara mkubwa na mkurugenzi wa kampuni moja kubwa ya madini ya nchini Uingereza wakati mama yake ni nesi katika hospitali moja nchini humo.

Mkasa wa mapenzi wa Colette ulianza miaka mitatu iliyopita wakati Colette alipoacha masomo yake ya chuo kikuu jijini Paris, Ufaransa na kuamua kuja Afrika kufanya kazi za kujitolea kwenye mashirika ya hisani.

Colette bila ya kumwambia mtu mwingine yeyote zaidi ya mama yake, ndani ya wiki moja aliacha shule na kufunga safari hadi Nairobi, Kenya kufanya kazi ya kujitolea kwenye taasisi ya watoto yatima.

Colette alitokea kupendwa kwenye taasisi hiyo ya yatima kutokana na jinsi alivyokuwa akijitolea kwa moyo wote kuwasaidia watoto yatima.

Colette alijipatia umaarufu wa ghafla baada ya mtoto wa miaka tisa aliyejulikana kwa jina la Mumbe ambaye hakuwahi kuongea hata siku moja kabla ya kuwasili kwa Colette, alipotamka neno la kwanza kumwita Colette "Mama".

Colette alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na tukio hilo akihesabika kama mtu mwenye miujiza.

Umaarufu huo ulipelekea chifu wa kimasai Kehmini kukitembelea kituo hicho cha yatima na kumpa mwaliko Colette wa kuitembelea jamii ya wamasai.

"Nilipofika nilionyeshwa kibanda ambacho kilikuwa hakina hata mlango, kulikuwa hakuna umeme wala maji", alisema Colette.

"Usiku sikulala kabisa nikihofia nyoka wataingia ndani na kunigonga, nilikuwa nikisiliza sauti toka kila kona kuhakikisha niko salama", aliongeza Colette.

"Maji ya kuoga nayo yalikuwa ya tabu nilishindwa kuoga kwenye mto kwa kuhofia mamba. Niliamua kuchota maji na kisha kuyachemsha kabla ya kuoga".

"Hata hivyo nilitokea kupenda maisha ya kimasai, wanaume wakiondoka asubuhi kwenda kuwinda wakiacha wanawake wakilea watoto, jioni tulikusanyika pembeni ya moto na kupiga stori", alisema Colette.

Ulikuwa ni wakati huo ndipo Colette alipoangukia kwenye penzi motomoto na kijana wa kimasai Meitkini mwenye umri wa miaka 23.

Colette alimaliza miezi akiishi kwenye boma la wamasai mpaka mwaka 2008 yalipotokea machafuko ya kisiasa nchini Kenya ambapo alishauriwa na maafisa wa umoja wa mataifa arudi kwao kwakuwa maisha yake yatakuwa hatarini kutokana na rangi yake.

Colette alikata shauri atumie muda huo kurudi Uingereza kumalizia masomo yake ingawa kutokana na mapenzi aliyo nayo ilikuwa vigumu kwake kuishi mbali na Meitkini.

Colette alirudi Uingereza na kumalizia masomo yake akiwataarifu pia wazazi wake na ndugu zake uamuzi wake wa kuolewa na mmasai na kuishi kwenye boma la wamasai.

Colette hakueleweka katika familia yake na wazazi wake waliliona suala hilo kama skendo na kuamua kutotaka kulizungumzia kabisa.

Colette ingawa hivi sasa ametengwa na wazazi wake bado ameshikilia msimamo wake wa kuolewa na Meitkini na yupo kwenye hatua ya mwisho ya kumalizia maandalizi ya harusi itakayofanyika siku chache zijazo.

Kuhusiana na suala la mumewe kuongeza mke mwingine kama jadi ya wanaume wa kimasai ilivyo, Colette anasema kuwa yeye hatajali kuwa mke mwenza ingawa anaamini Meitkini hafikirii kuongeza mke mwingine zaidi yake.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment