Kuku Mwenye Hirizi Tatu Atinga Hospitali ya Muhimbili

Wednesday, April 07, 2010 / Posted by ishak /

Kuku mwenye hirizi tatu za rangi tofauti alizua kizaa zaa alipoonekana kwenye maeneo ya hospitali ya Muhimbili na baadae kuingia kwenye madarasa ya chuo kikuu cha Muhimbili.
Kuku huyo mweusi alikuwa amevishwa hirizi zenye rangi tatu tofauti nyeusi, nyekundu na nyeupe.

Alionekana kwenye maeneo ya Chuo Kikuu cha Muhimbili kilichopo kwenye hospitali hiyo kubwa nchini Tanzania.

Kuku huyo aliwafanya walinzi wa eneo hilo wachanganyikiwe wasijue la kufanya baada ya kumshuhudia kuku huyo mweusi akirandaranda kwenye maeneo ya Hospitali ya Muhimbili akiwa na hirizi zake tatu.

Haikujulikana mara moja kuku huyo ni wa nani au alitokea wapi ila mmoja wa walinzi wa Muhimbili alisikika akisema eneo hilo limekuwa na matukio mengi ya aina hii na haifahamiiki ni kwanini inakuwa hivyo.

Hata hivyo walinzi wa Muhimbili hawakupenda kulizungumzia suala la kuku huyo wa ajabu.

Watu waliokusanyika waliamrishwa waondoke kwenye eneo la tukio na walinzi kutakiwa warudi kwenye malindo yao baada ya mmoja wa walinzi kumpiga picha kuku huyo kwaajili ya ushahidi na kumbukumbu ya tukio hilo.


source nifahamishe