Ng'ombe Anapobebwa Kwenye Ambulansi....

Sunday, April 04, 2010 / Posted by ishak /


Si jambo geni nchini Tanzania kuona gari la serikali likiwa limebeba majani ya ng'ombe au likifanya shughuli ambayo ipo nje ya matumizi ya kikazi, kali ya yote imetokea nchini Pakistan baada ya daktari kununua ng'ombe kwenye mnada na kumpakiza ng'ombe kwenye ambulansi.
Afisa wa kitengo cha afya nchini Pakistan amesimamishwa kazi baada ya kutumia gari la ambulansi kubebea ng'ombe wake aliyemnunua kwenye mnada wa ng'ombe.

Dr Munir Ahmed, afisa wa kituo cha afya cha kitongoji cha Tanda nchini Pakistan amefukuzwa kazi baada ya kutumia gari la ambulansi kumsafirisha ng'ombe wake aliyemnunua kwenye mnada uliopo kilomita 10 toka mji wa Gujrat.

Askari wa usalama wa barabarani waliisimamisha ambulansi hiyo baada ya kuona ng'ombe akiwa ndani huku maski za oxygen zikining'ia kwenye ambulansi hiyo.

Gazeti la Dawn la nchini Pakistan lilichapisha picha ya ng'ombe huyo akiwa ndani ya ambulansi kwenye sehemu ya nyuma ambayo kawaida wagonjwa hulazwa wakati wakiwahishwa hospitali.

Dr. Munir alisimamishwa kazi muda mfupi baada ya kuchapishwa kwa picha hiyo kwenye gazeti huku uchunguzi zaidi ukifanyika kuhusiana na tukio hilo.


source nifahamishe