Afukuzwa Kazi Kwasababu ya Urembo Wake

Friday, June 04, 2010 / Posted by ishak /


Mwanamke mmoja nchini Marekani amefukuzwa kazi kwasababu ni mrembo sana na nguo za kazi anazovaa zinawachengua wafanyakazi wenzake wa kiume.
Debrahlee Lorenzana mama wa mtoto mmoja alikuwa mfanyakazi wa benki ya Citibank lakini umbo lake namba nane na urembo wake ulikuwa ukiwachanganya wafanyakazi wenzake wa kiume kiasi cha kuzorotesha ufanisi wao wa kazi.

Debrahlee mwenye umri wa miaka 33 aliambiwa kwamba nguo za kazini anazovaa kama wafanyakazi wenzake wa kike zinawachengua mabosi wake kiume na wafanyakazi wenzake.

Baada ya malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi wanaume, mabosi wake walimshauri Debrahlee asivae baadhi ya viwalo vya kazini kwakuwa vinamfanya aonekane mrembo zaidi.

Debrahlee alipeleka malalamiko kwenye menejimenti ya benki hiyo akiuliza sababu ya kuzuiwa kuvaa nguo ambazo wafanyakazi wenzake wanaruhusiwa kuvaa.

Katika majibu aliyopewa kufuatia malalamiko yake hayo, Debrahlee aliambiwa kuwa wafanyakazi wenzake wa kike wanaweza wakavaa chochote wakipendacho kwakuwa hawana mvuto.

Aliambiwa pia kwakuwa yeye ana umbile namba nane na ameenda hewani sekunde, asivae viatu vyenye soli ndefu kwakuwa vinalifanya umbile lake lionekane vizuri hivyo kuwachanganya zaidi mameneja wake wanaume.

Baada ya miezi 10 katika benki hiyo, Debrahlee alihamishwa kikazi na kupelekwa kwenye tawi jingine la benki hiyo lakini huko alifukuzwa kazi ndani ya mwezi mmoja akiambiwa kuwa ana ufanisi mdogo.

Debrahlee ameenda mahakamani kupinga kufukuzwa kazi.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment