Mapenzi Yanapozidi..

Friday, June 04, 2010 / Posted by ishak /


Mwanaume mmoja wa nchini Uingereza kwa uchungu aliokuwa nao wa kuondokewa na mpenzi wake, aliamua kuishi na maiti ya mpenzi wake ndani ya nyumba yake akiimwagia pafyumu nyingi sana ili kuzuia harufu isitoke nje.
Gabriel Brown, 54, aliishi na maiti ya mpenzi wake akiiweka kwenye kochi na kuyanyunyuzia pafyumu mabaki yake ya mwili wake ambao uliendelea kuoza ili kuzuia harufu isitoke nje ya nyumba yake.

Gabriel aliishi hivyo kwa takribani miezi 10 hadi alipotiwa mbaroni mwezi disemba mwaka jana baada ya maiti ya mpenzi wake Lynn Warman, 37, ilipokutwa kwenye kochi nyumbani kwake ikiwa imezungukwa na makopo ya pafyumu.

Brown aliwaambia polisi kuwa mpenzi wake alifariki februari 9, 2009 lakini kutokana na majonzi aliyokuwa nayo hakutaka kutoa taarifa polisi.

Brown alishikiliwa na polisi kama mtuhumiwa wa kifo cha mpenzi wake lakini aliachiwa kwa dhamana wakati polisi wakiendelea na uchunguzi.

Wakati polisi wakiendelea na uchunguzi kutafuta ukweli wa kifo cha mpenzi wake, Brown naye alikutwa amefariki baada ya kupoteza damu nyingi wakati alipopata ajali.

Uchunguzi wa maiti ya Lynn ulionyesha kuwa hakuuliwa na alifariki akiwa amekaa kwenye kochi ambalo maiti yake ilikutwa.

Mmoja wa majirani zake alisema: "Brown na Lynn walikuwa wakipendana sana, inasikitisha kusikia kwamba maiti ya Lynn ililala kwenye kochi karibia mwaka huku Brown akiishi nyumba hiyo hiyo".

"Sijui aliwezaje kuishi kwenye harufu mbaya ya maiti iliyoharibika, Natumaini watapumzika kwa amani huko waliko", aliongeza kusema jirani huyo.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment