Watoto Wafariki Wakati Baba na Mama Wakiangalia Kombe la Dunia

Wednesday, June 16, 2010 / Posted by ishak /


Watoto wawili wamefariki dunia nchini Uganda kutokana na moto ulioitekeza nyumba yao wakati wazazi wao walipoenda kwa jirani mwenye televisheni kuangalia kombe la dunia.
Polisi mjini Kampala nchini Uganda wamesema kuwa watoto wawili wamefariki kutokana na moto ulioitekeza nyumba yao wakati wazazi wao walipoenda kuangalia mechi ya kombe la dunia.

Polisi nchini Uganda wamewaonya wazazi kutowaacha watoto wao peke yao ndani ya nyumba wakati wanapoenda kuangalia mechi za kombe la dunia.

Watoto wawili wenye umri wa miaka 8 na 10 walifariki kwa moto katika wilaya ya Kayunga iliyopo magharibi mwa mji wa Kampala.

Afisa wa polisi wa Kayunga, Henry Kolyanga alisema kuwa watoto hao walifariki wakati nyumba waliyokuwa wamelala iliposhika moto.

"Mama na Baba wa watoto hao waliacha mshumaa ukiwaka ndani ya nyumba na walienda kuangalia mechi ya kombe la dunia kwa jirani mwenye televisheni", alisema afisa huyo wa polisi.

"Inasemekana kuwa panya aliugonga mshumaa na mshumaa huo uliangukia kwenye meza na kukiunguza kitambaa cha mezani na kusababisha moto mkubwa ulioitekeza nyumba yote", alimalizia kusema afisa huyo wa polisi.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment