Kutokana na wivu mwanamke mmoja nchini Marekani alimchoma moto mpenzi wake na kisha kujichoma moto na yeye mwenyewe na kutokana na moto huo nyumba ilishika moto na kupelekea vifo vya watu wengine watatu.
Agnes Bermudez, 50, anatuhumiwa kumuua mpenzi wake William Salazar, 32, katika tukio la kutisha lililotokea siku ya akina baba duniani mwaka 2008.
Agnes ambaye hivi sasa kesi yake inaendelea mahakamani, alimchoma moto mpenzi wake huyo na kisha yeye mwenyewe alijipiga kibiriti.
Agnes hakufariki kutokana na moto aliouanzisha lakini aliungua vibaya sura yake kiasi cha kumfanya asitambulike.
Sababu ya Agnes kumchoma moto mpenzi wake ni wivu wa kimapenzi. Agnes alimshutumu Salazar kuwa anatembea na mwanamke mwingine nje.
Video ya tukio hilo imetolewa mahakamani kama ushahidi wa tukio hilo la kusikitisha.
Video inamuonyesha Agnes na Salazar wakitoka nje ya nyumba yao wakikimbilia kwenye duka lililopo chini ya jengo lao.
Salazar anaonekana akikimbia kuingia ndani ya duka akitafuta maji wakati Agnes alilala chini mbele ya duka hilo huku akiungua na moto.
Wasamaria wema walifanikiwa kuwamwagia maji na kuokoa maisha yao hata hivyo Salazar alifariki siku nne baadae hospitalini.
Moto ulioanzishwa na Agnes ulishika pia nyumba zingine zilizopo kwenye jengo hilo na kupelekea vifo vya watu watatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment