Wakati wanawake katika nchi za magharibi wanapigania kuwa na matiti makubwa hali ni tofauti nchini Cameroon ambapo akina mama nchini humo wanatumia njia ya kikatili ya kuyapiga pasi matiti ya watoto wao wa kike ili kuwaepusha wasibakwe.
Ili kuwafanya wanaume wakware wasianze kuwanyemelea mabinti zao wanapoanza kupevuka na kupelekea mimba zisizohitajika, akina mama nchini Cameroon wanatumia njia inayosababisha maumivu makali sana ya kuyapiga pasi matiti ya watoto wao wa kike ili yaendelee kuwa madogo wakati wote na hivyo kutowavutia wanaume.
Njia hiyo inayojulikana kama "Breast ironing" hufanyika kwa mawe kuwekwa kwenye moto na kisha mawe hayo kukandamizwa kwenye chuchu ili kuyafanya matiti yasiendelee kuongezeka ukubwa.
Njia hiyo husababisha maumivu makali kwa watoto wa kike na hupelekea baadhi yao wapate vilema vya maisha na wengine washindwe kuwanyonyesha watoto wao wanapokuwa wakubwa.
Utafiti unaonyesha kuwa watoto wa kike nchini Cameroon huanza kupevuka wanapokuwa na umri wa miaka tisa na ni wakati huo huo mama zao huanza kuzipiga pasi chuchu zao ili wasiwavutie wanaume.
Pamoja na njia hiyo kuonekana ya kikatili sana na yenye kuwasababishia maumivu na majeraha watoto wa kike, akina mama nchini Cameroon wanaitetea njia kwa kusema kuwa inawaepusha watoto wao kupata mimba mapema.
source nifahamishe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment