Operesheni za Kurudisha Bikira Zawa Dili Uingereza

Friday, July 30, 2010 / Posted by ishak /


Wanawake waliozipoteza bikira zao kwa ngono ambao wanataka kuzirudisha bikira zao kabla ya kuolewa wamezidi kuongezeka nchini Uingereza ambapo operesheni za kurudisha bikira zimekuwa zikifanyika kwa wingi sana siku hizi.
Maelfu ya wanawake nchini Uingereza ambao hutaka waonekane ni bikira kwa waume zao, wamekuwa wakifanya operesheni za kuzirudisha bikira zao.

Idadi ya operesheni za kurudisha au kurekebisha bikira zinazofanyika kwenye mahospitali nchini Uingereza zimeongezeka kwa kasi katika miaka ya karibuni ambapo wanawake wamekuwa wakilipa hadi paundi 4,000 (Takribani Tsh. Milioni 9).

Operesheni hizo zinazotumia muda wa nusu saa huzirudisha tishu za hymen (ngozi inayoziba mlango wa uke) na kumfanya mwanamke awe bikira kwa mara nyingine tena.

Bikira hiyo ya kutengeneza nayo huwa na uwezo wa kuchanika na kutoa damu mwanamke anapojamiiana kwa mara ya kwanza baada ya operesheni hiyo.

Mmoja wa madaktari wa hospitali moja binafsi nchini Uingereza alisema kuwa idadi kubwa ya wanawake wanaoenda kwake ni wanawake wenye asili ya bara la Asia ambao hutaka kuwahakikishia waume zao kuwa hawajawahi kufanya mapenzi kabla ya usiku wa harusi yao.

"Ni jambo la kitamaduni zaidi kuliko kidini, kama mwanamke hatatoa damu kwenye kitambaa cheupe usiku wa harusi yake, basi huonekana ameidhalilisha na kuitia aibu familia yake", alisema daktari huyo.

"Mwanamke huhofia kuwa mumewe anaweza akatoa talaka au kuitolea kashfa familia yake au kumnyanyasa maisha yake yote iwapo atajulikana si bikira", aliongeza daktari huyo.

Daktari huyo aliongeza kuwa wanawake wanaofanya operesheni za kurudisha bikira zao wengi wao hutumia majina na anuani feki ili wasijulikane.

source nifahamishe