Bomba la Mafuta Lapasuka Dar, Watu Wagombania Mafuta

Monday, July 26, 2010 / Posted by ishak /


Baada ya bomba la mafuta kupasuka baharini nchini Marekani na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira, bomba la mafuta la TIPA katika bahari ya Hindi limepasuka lakini tofauti na hali ilivyokuwa nchini Marekani Watanzania waligombania kuchota mafuta.
Bomba la mafuta la TIPA na Orexy limepasuka na kusababisha mafuta ya Disel kumwagika katika ufukwe wa Kivukoni na kusababisha shughuli za uoshaji wa samaki kusimama kwa takribani siku nzima.

Akizungumuzia tukio hilo Katibu wa Wizara ya Miundombinu Omary Chande amesema kuwa tatizo lililojitokeza katika bomba hilo la mafuta ni bomba dogo ambalo limepasuka katika mabomba ya Tipa na Orexy ambayo yapo umbali kidogo kutoka katika kivuko cha magogoni.

Baada ya kupata taarifa ya kupasuka kwa mabomba hayo, mafundi wa TIPA walizama ndani ya maji hayo na kuanza kuziba bomba hilo na hatimaye walifanikiwa kuliziba bomba hilo.

Mamia ya vijana wanaojazana maeneo ya feri walikimbilia eneo la tukio ambapo walianza kazi ya kuchota mafuta yaliyokuwa yakielea juu ya maji.

Mafuta yaliyopatikana toka eneo hilo yalikuwa yakiuzwa kwa madereva wa madalala ambapo lita tano kwa kiasi cha shilingi 5,000.

Vijana wasio na ajira ambao mara zote hushinda hapo feri wamesema hii ni neema kwao kwasababu kwa jana pekee wameweza kujipatia kipato kikukbwa ambacho hawakuweza kukitegemea kupata na wanaomba hali hii ingeendelea kutokea kila siku.

Lakini hali ilikuwa tofauti kwa waosha samaki kwani kwa siku ya leo hawakuwa na kazi kutokana na bahari yote kujaa mafuta ya disel ambayo yalikuwa yakinuka kila sehemu.

Katibu Chande alisema kutokana na uharibifu wa mazingira uliotokea, ofisi yake kwa kushirikana na wahusika tayari wameweka dawa kwa ajili ya kudhibiti ukali wa mafuta na kusababisha yasiwe na nguvu yoyote ya kudhuru wananchi.

Pia aliwataka watumiaji wa magari wanaonunua mafuta yaliyochotwa kwenye eneo hilo, wasiyatumie mafuta hayo maana tayari yameshaharibiwa kwa kutumiwa dawa maalumu.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment