Ajali Yasababisha Awe na Hamu ya Mapenzi Wakati Wote

Thursday, December 17, 2009 / Posted by ishak /


Mwanamke mmoja wa nchini Marekani maisha yake yamebadilika baada ya kupata ajali ambayo imesababisha awe na hamu ya kufanya mapenzi muda wote. Msuguano wa nguo na mwili wake husababisha awe kwenye kilele cha mapenzi bila hata kuguswa na mwanaume yoyote.
Kutokana na ajali ya gari ambayo ilisababisha madhara kwenye mishipa ya fahamu inayokatiza kwenye nyonga yake, Joleen Baughman mwenye umri wa miaka 39 amekuwa akikabiliwa na hali ambayo humtesa masaa 24 ya kila siku.

Ajali hiyo iliyotokea miaka miwili iliyopita, ilisababisha mshipa wa fahamu uliopo kwenye nyonga ambao husimamia matamanio ya kimapenzi ya binadamu uwe kama umeachiliwa kufanya kazi muda wote.

Wakati wote Joleen hutamani kufanya mapenzi bila hata kutosheka.

Kutokana na hali hiyo, kitendo cha kukaa kwenye kiti, kuinama na hata kutembea ndani ya chumba chake husababisha mambo yawe si mambo kwenye nyeti zake bila hata kuguswa na mtu yoyote sehemu hizo.

Joleen ambaye ni mama wa watoto wawili mkazi wa New Mexico, Marekani alisema "Ni hali ambayo nashindwa kujizuia, hata msuguano wa nguo nilizovaa na mwili wangu husababisha niwe kwenye hamu kubwa sana ya kufanya mapenzi".

Joleen ambaye anaishi na mumewe Brian, 39, na watoto wao wawili anakabiliwa na ugonjwa unaowapata watu wachache sana unaoitwa "Restless Genital Syndrome".

Joleen alipata ajali mwezi aprili mwaka 2007 wakati alipokuwa kwenye gari na mumewe na gari lao kugongana uso kwa uso na gari la mwanaume aliyekuwa amelewa madawa ya kulevya.

Joleen alilazwa hospitali wiki kadhaa baada ya kufanyiwa operesheni ya ubongo na uti wake wa mgongo ambao nao ulivunjika katika ajali hiyo.

Alipona taratibu na kuruhusiwa kurudi nyumbani kwake lakini baada ya miezi sita madhara ya ajali hiyo yalianza kujitokeza.

Joleen ambaye awali alikuwa sio mpenzi sana wa kufanya mapenzi, alianza kushikwa na hamu ya ajabu ya ngono muda wote.

Awali yeye na mumewe wa ndoa ya miaka 20 walifurahia hali hiyo kwa kuwa mumewe alikuwa akipenda sana kufanya tendo la ndoa.

"Brian alikuwa na furaha kwamba kwa mara ya kwanza katika ndoa yetu mimi ndio nalazimisha kufanya mapenzi muda wote", alisema Joleen.

"Ndani ya siku moja kwa mfano tungefanya mara ya kwanza, tuliporudia mara ya pili ndio kwanza hamu yangu ya kimapenzi huanza kuongezeka, tunapoenda raundi ya tatu huwa nahisi maumivu lakini nakuwa na hamu kuliko mwanzo".

Baada ya kugundua kuwa kufanya mapenzi mara nyingi hakutatibu tatizo lake, Joleen alianza kutafuta tiba ya tatizo lake.

Alikata tamaa baada ya madaktari kumwambia kuwa tatizo lake si la kisaikolojia bali linatokana na mshipa wa fahamu unaoitwa pudendal uliopo kwenye nyonga karibu na sehemu za siri.

Kutokana na ugonjwa huo kutokuwa na tiba maalumu, Joleen bado anaendelea kusumbuliwa na tatizo hilo hadi leo.

source.nifahmishe.com

0 comments:

Post a Comment