Duka La Kwanza la Ngono la Kiislamu Lazinduliwa

Wednesday, March 31, 2010 / Posted by ishak /


Duka la kwanza la bidhaa za ngono zinazodaiwa kuwa ni 'HALAL' limezinduliwa kwaajili ya waislamu nchini Uholanzi na baadhi ya mashehe wametoa ruhsa ya duka hilo la kwenye internet wakisema kuwa halivunji sheria za kiislamu.
Duka hilo linalodaiwa kuwa duka la kwanza duniani kwaajili ya waislamu wanaohitaji bidhaa za kuchombeza mapenzi yao lilizinduliwa wiki iliyopita.

Ndani ya siku nne za kuzinduliwa kwa mtandao wa tovuti hiyo kulikuwa na jumla ya cliks 70,000, alitamba mmiliki wa tovuti hiyo ya kwanza ya bidhaa za ngono kwaajili ya waislamu, Abdelaziz Aouragh.

Tovuti hiyo inayoitwa "El Asira" kwa maana ya jamii katika lugha ya kiarabu, ilizinduliwa kwa lengo la kuwauzia wanandoa wa kiislamu bidhaa za erotika.

Abdelaziz ambaye ni raia wa Uholanzi mwenye asili ya Moroko alisema kuwa alianzisha duka hilo la kwenye mtandao ili kuwaepusha waislamu kuingia kwenye tovuti zinazouza bidhaa hizo ambazo huweka picha na video za ngono ambazo ni haramu katika uislamu.

Ukurasa wa mbele wa El Asira hauna kitu chochote zaidi ya mstari unaotenganisha wanawake na wanaume, wanawake hutakiwa kuclick upande wao wa kushoto na wanaume huingia upande wa kulia.

Tovuti hiyo ina lugha tatu za kidachi, kiarabu na kiingereza na huuza zaidi mafuta kwaajili ya masaji, mafuta ya kupunguza ukinzani (lubricants) na dawa mbali mbali za malavi davi.

"Kila kinachopatikana humu ni Halal kinaruhusiwa katika uislamu' alisema Abdelaziz na kuongeza kuwa hakuna picha wala video za ngono kwenye tovuti yake.

Tovuti hiyo inaonyesha bidhaa zikiwa zimepigwa picha kwenye maboxi yake.

Abdelaziz alisema kuwa kabla ya kuanzisha duka hilo la kwenye mtandao alipata ushauri toka kwa mashehe mbalimbali na wanazuoni wa Uholanzi na Saudia ambao walimwambia kuwa hakuna sheria ya kiislamu anayoivunja.

"Ili mradi hauzi toys za ngono au vitu kama hivyo, hakuna tatizo lolote", alisema imamu wa Uholanzi, Abdul Jabbar.

"Mtume Muhammad (s.a.w) alitoa ushauri mbalimbali kuhusiana na masuala ya mapenzi kwenye ndoa, hivyo hakuna kitu cha kukionea aibu", aliongeza imamu huyo.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment