Mchungaji Chapombe Asababisha Kasheshe Makaburini

Friday, April 02, 2010 / Posted by ishak /


Askofu wa kanisa katoliki nchini Ufaransa ameomba radhi kufuatia kitendo cha mchungaji mmoja wa kanisa hilo kuongoza mazishi makaburini akiwa amelewa na kumtwanga ngumi ya uso mmoja wa waombelezaji.
"Mchungaji Bonaventure aliwasili makaburini akiwa amelewa katika hali ambayo haiendani na tararibu za kanisa", alisema askofu Robert le Gall katika taarifa yake ya kuwaomba radhi familia ya marehemu.

Ndugu wa mwanamke aliyefariki walielezea jinsi walivyomtaka mchungaji huyo ambaye ni raia wa Burkina Faso kuwa hawataki aongoze misa ya mazishi ya ndugu yao kwakuwa alikuwa amelewa sana.

Katika mazishi hayo yaliyofanyika siku ya jumanne katika mji wa Toulouse uliopo kusini magharibi mwa Ufaransa, mchungaji huyo alikubali kuondoka lakini alipotaka kuendesha gari lake mwenyewe, ndugu wa marehemu walijaribu kumzuia kwakuwa alikuwa hajiwezi hata kutembea akianguka chini mara kwa mara.

Kuna wakati mchungaji huyo alidondoka chini na mmoja wa waombelezaji alipojitolea kumuinua mchungaji huyo alimtandika ngumi ya uso, alisema Gerard Tillier ambaye ni kaka wa marehemu.

"Mchungaji gani huyu anakuja kwenye mazishi akiwa amelewa na kuwapiga ngumi waumini wake? ", alisema kaka huyo wa marehemu

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment