Mwanamke wa nchini Kuwait ambaye alianzisha moto kwenye harusi kupinga mumewe kuoa mke mwingine na kupelekea vifo vya watu 57 amehukumiwa adhabu ya kifo.
Akitoa hukumu dhidi ya Nasra Yussef Mohammed al-Enezi, 23, jaji Adel al-Sager aliamuru Nasra auliwe kwa kitendo chake cha kuanzisha moto kwenye hema wakati wa sherehe za harusi na kupelekea vifo vya watu 57.
Nasra alipatikana na hatia ya kulichoma moto hema ambalo wanawake na watoto walikuwa wamekaa wakati wa harusi ya mumewe akiongeza mkewe mwingine.
Moto katika tukio hilo la mwezi wa nane mwaka jana, uliwateketeza wanawake na watoto ndani ya dakika 10 tu na ulisababisha majeruhi kadhaa.
Nasra alianzisha moto huo ili kupinga mumewe kuongeza mke mwingine.
Nasra alikamatwa siku moja baada ya wanawake 41 na watoto kufariki kwenye moto uliozuka kwenye hema katika mji wa Jahra uliopo magharibi mwa Kuwait. Idadi ya vifo iliongezeka baadae na kufikia 57.
Awali ilidaiwa kuwa alikuwa amepewa talaka na mumewe lakini wakili wa utetezi walisema kuwa alikuwa bado ni mke wa bwana harusi huyo na alikuwa na mimba ya miezi miwili ambayo mawakili wake wanadai ilitolewa alipokuwa jela.
Nasra na mumewe walikuwa na watoto wawili ambao wote walikuwa na matatizo ya akili.
Mawakili wa Nasra wamesema watakata rufaa ya hukumu hiyo mahakama kuu.
source nifahamishe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment