Maiti za Watoto Zatupwa Kwenye Mto

Wednesday, March 31, 2010 / Posted by ishak /


Wafanyakazi wawili wa monchwari nchini China wanashikiliwa na polisi baada ya kuzitupa maiti 21 za watoto kwenye mto.
Wafanyakazi wawili wa ngazi za juu wa hospitali moja nchini China wamefukuzwa kazi huku wafanyakazi wawili wa monchwari wakiwa mbaroni baada ya maiti 21 za watoto kuopolewa toka kwenye mto.

Maiti za watoto wanane zilikuwa na alama za kuonyesha kuwa zilikuwa zimehifadhiwa kwenye hospitali ya chuo kikuu cha Jining Medical University katika mji wa Shandong, limeripoti shirika la habari la Xinhua.

Taarifa zinasema kuwa maiti za watoto hao zilikuwa ni za vichanga vilivyouliwa wakati wa utoaji mimba na watoto waliofariki kutokana na maradhi mbali mbali.

Taarifa za polisi zinasema kuwa wafanyakazi hao wa monchwari walilipwa na ndugu wa watoto waliofariki wazizike maiti za watoto hao lakini wao waliamua kuzitupa kwenye mto ulio mbali sana na hospitali hiyo.

Maiti za watoto zikiwa katika mifuko ya rambo ya njano ziliopolewa toka kwenye mto na kuzua hasira za wananchi walioshuhudia tukio hilo.


source nifahamishe