Ndege Yadondoka Rais Wa Poland Afariki

Sunday, April 11, 2010 / Posted by ishak /


Rais wa Poland, Lech Kaczynski pamoja na mkewe na maafisa wa jeshi na serikali wamefariki dunia baada ya ndege iliyokuwa imebeba abiria 132 kuanguka karibu na uwanja wa ndege nchini Urusi.
Rais Lech Kaczynski wa Poland amefariki dunia kufuatia ajali mbaya ya ndege iliyotokea leo baada ya ndege yake kuanguka kwenye miti karibu na uwanja wa ndege wa Smolensk nchini Urusi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, abiria waote 132 waliokuwemo kwenye ndege hiyo wamefariki dunia.

Miongoni mwa wwaliofariki katika ajali hiyo ni mke wa rais huyo, Maria, Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Andrzej Kremer, Mkuu wa majeshi ya Poland, Franciszek Gagor, na Gavana wa Benki Kuu ya nchi hiyo, Slawomir Skrzypek.

Pia katika orodha ya watu waliofariki kutokana na ajali hiyo ya ndege ni wabunge wa Poland na wanahistoria kadhaa.

Rais huyo wa Poland pamoja na ujumbe wake walikuwa wakielekea katika mji wa Katyn karibu na Smolensk kuhudhuria kumbukumbu ya mauaji ya wafungwa wa vita wa Urusi na Poland waliouawa wakati wa utawala wa kisovieti.

Kufuatia kifo hicho, Spika wa bunge la Poland, Bronislaw Komorowski, anachukua madaraka ya nchi hiyo.

Rais Kaczynsk na mkewe ambao wote wamefariki katika ajali hiyo wameacha mtoto mmoja wa kike, Marta.

source nifahamishe