Watu 11 wamefariki nchini Senegal na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya jengo walilojazana kuangalia mpira kuporomoka.
Polisi nchini Senegal wamesema kuwa watu 11 wamefariki dunia wakiangalia mechi ya kombe la dunia wakati jengo walilokuwemo lilipobomoka na kuwafunika.
Kundi kubwa la watu lilikusanyika kwenye nyumba ya mkuu wa kampuni ya umeme katika mji wa Matam kaskazini mwa Senegal ili kuangalia mechi ya kombe la dunia.
Polisi walisema kuwa jengo hilo lilibomoka wakati wakati wa mechi ya jumamosi mchana kati ya Uruguay na Korea.
Senegal haikufanikiwa kufuzu kushiriki fainali za kombe la dunia lakini fainali za kombe za dunia zinazoendelea nchini Afrika Kusini zimekuwa zikifuatiliwa kwa ukaribu sana nchini humo.
Mamia ya watu walimiminika mitaani jumamosi usiku kushangilia ushindi wa Ghana wa mabao 2-1 dhidi ya Marekani.
Ghana ndio wawakilishi pekee wa Afrika waliobaki kwenye kombe la dunia na wataingia uwanjani ijumaa kumenyana na Uruguay ili kuwania tiketi ya nusu fainali.
source nifahamishe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment