HOSPITALI ya Wilaya ya Ilala Amana ya Dar es Salaam, imemkabidhi Martin [35] mtoto Alphonce Martin aliyekuwa akilelewa hapo kwa takribani siku 11 baada ya uthibitisho wa kina kuwa ni mwanae halali
Martin Melicyori mkazi wa Pugu Kinyamwezi, akifuatana na ndugu zake aliweza kukabidhiwa mtoto huyo kwa kuwasilisha barua ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa anapoishi kuthibitisha kuwa ni mwanae na kufafanua maswali aliyopewa hospitalini hapo.
Mbali na kuwasilisha maelezo hayo pia aliweza kutoa ushahidi mwengine mbalimbali ikiwemo picha mbalimbali na kufafanua vizuri maswali aliyokuwa akihojiwa.
Martin alidai kwa kweli hakuwa na habari kabisa kama mkewe alifikishwa hospitalini hapo kwa kuwa siku ya mwisho mkewe alimuaga kwenda kutafuta huduma za uzazi wa mpango akiwa na jirani yake.
Alisema kuwa majira ya jioni jirani yake huyo alifika nyumbani kwake na kumuulizia mke wake kama alikuwa amerudi na kumshanga kwa kuwa waliondoka wote na kutoa taarifa kituo cha polisi.
Alisema alijitahidi kufika hospitali mbalimbali hadi Muhimbili na kuambiwa hakuna jina la la mgonjwa kama huyo na hadi juzi walipoona taarifa hiyo kwenye gazeti.
KAtika maelezo yake alisema kuwa Alphonce ni motto wake wa tatu kuzaliwa kati ya watoto watatu ikiwa ni pamoja na Sweet (9) na Samson (4.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dk. Meshark Shimwela, baada ya kuridhika na maelezo hayo pia ndugu hao waliruhusiwa kuja kuchukua mwili wa marehemu ambao ulikuwa umehifadhiwa hospitalini hapo ilipowasiliana na uongozi wa hospitali hiyo ulidai kuwa mwili huo utachukuliwa leo kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Tabata.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment