Amuua Mtoto Wake Kwa Hasira za Marekani Kufungwa na Ghana

Thursday, July 01, 2010 / Posted by ishak /


Mwanaume mmoja nchini Marekani anashikiliwa na polisi baada ya kumpiga mpaka kumuua mtoto wake aliyekuwa akilia sana wakati yeye akiangalia mechi ya kombe la dunia kati ya Marekani na Ghana ambayo Marekani ilifungwa 2-1 na kuliaga kombe la dunia.
Hector Castro mwenye umri wa miaka 28 alimpiga sana na kisha kumuua kwa kumziba pumzi mtoto wake wa kambo wa kike mwenye umri wa miaka miwili.

Baada ya kumuua mtoto huyo ili kuficha ukweli, Castro aliididimiza bisibisi kwenye shingo ya mtoto huyo ili kufanya kifo cha mtoto huyo kionekane kuwa ni cha ajali.

Castro aliita ambulansi akidai mtoto wake amepata ajali wakati akicheza na bisibisi imezama kwenye shingo yake.

Hata hivyo mchezo wake uligundulika muda mfupi baada ya madaktari waliokuja na ambulansi kugundua kuwa mtoto huyo alifariki kutokana kupigwa na kuvunjwa mbavu kadhaa na wala si bisibisi.

Castro alitiwa mbaroni kwa tukio hilo lililotokea jumamosi wakati wa mechi ya kuwania kuingia robo fainali kati ya Marekani na Ghana.

Castro alijitetea kuwa alishikwa na hasira kutokana na mtoto huyo kulia sana bila kunyamaza wakati yeye akiangalia mechi hiyo ya Marekani na Ghana ambayo iliisha kwa Marekani kufungwa mabao 2-1.

Kutokana na umri mdogo wa mtoto aliyeuliwa, Castro huenda akahukumiwa adhabu ya kifo iwapo atapatikana na hatia.
source nifahamishe