Baada ya bunge la Iceland kuipitisha sheria ya kuruhusu watu wa jinsia moja kuoana, waziri mkuu wa Iceland ambaye ni mwanamke amefunga ndoa na mwanamke mwenzake.
Waziri mkuu wa Iceland, bi Johanna Sigurdardottir amefunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi ambaye pia ni mwanamke.
Siku chache baada ya bunge la Iceland kupitisha sheria ya kuruhusu watu wa jinsia moja kuoana, bi Johanna amefunga ndoa na mpenzi wake Jonina Leosdottir.
Bi Johanna amekuwa akiishi na Jonina kwa muda mrefu na walifunga ndoa juzi jumapili.
Sheria ya kuruhusu wanaume kuoa wanaume wenzao na wanawake kuoa wanawake wenzao ilipitishwa juni 11 mwaka huu bila ya upingamizi wowote.
Bi Johanna mwenye umri wa miaka 66 alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Iceland mwaka jana baada ya migomo iliyosababishwa na kutetereka kwa uchumi kupelekea serikali iliyokuwepo kuondolewa madarakani.
Bi Johanna ndiye waziri mkuu wa kwanza barani ulaya kujitangaza wazi kuwa yeye ni msagaji. Ndoa yake inaonekana itakuwa ni changamoto kwa jumuiya zinazounga mkono ndoa za jinsia moja.
source nifahamishe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment