11 mbaroni sakata la vifo vya watoto Luxury Pub

Wednesday, September 15, 2010 / Posted by ishak /

KUFUATIA ripoti maalum iloyoundwa kuchunguza sababu iliyopelekea kutokea kwa vifo vya watoto na kubainika ni uzembe ulisababisha vifo hivyo, watu 11 wanashikiliwa na polisi.
Ripoti hiyo imeonyesha kuwa uzembe mkubwa ulifanyika katika ukumbi huo na kusababisha vifo hivyo.

Akitoa ripoti hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bi. Chiku Galawa alisema, ripoti hiyo imeonesha kuwa uzembe uliofanyika katika ukumbi huo ni kuwa na idadi kubwa ya watu ndani ya ukumbi huo kuliko uwezo wa ukumbi.

Pia mmiliki wa ukumbi huo imegundulika hakuwa na kibali cha kuendesha biashara hiyo ya disco hivyo alikuwa akienda kinyume na sheria za nchi, na aliendesha dico hilo toto hadi majira ya saa 1:50 usiku na kuonekena kukiuka utaratibu uliowekwa.

"Watoto ni haki yao kufurahia sikukuu, lakini mmiliki wa ukumbi huo alikiuka maadili ya watoto, kwanza aliwalundika watoto ukumbini kupit kiasi, pili alipitisha muda maalum" alsiema mkuu huyo

Mmiliki wa ukumbi huo alitambulika kwa jina la Damas Nyingo alikuwa ni mmoja kti ya watu 11 waliokamatwa na majina mengine hayakuekwa bayana hadi upelelezi ukamilike.

Watoto wawili waliweza kupoteza maisha sikukuu ya Idd Pili, katika ukumbi wa Luxury Pub uliopo Temeke, katika makutano ya mtaa wa Madenge na Liwale baada ya umeme kukatika ghafla na kusababisha watoto kukimbia hovyo mlangoni na kukanyagana.

Watoto waliopoteza maisha ktika tukio hilo ni Lilian Sango (8) na Amina Ramadhani (7), wote wakazi wa Temeke na wengine zaidi ya kumi na moja kujeruhiwa.

source nifahamishe