Aamua Kumuoa Dada Yake

Wednesday, September 15, 2010 / Posted by ishak /


Mwanaume wa nchini Ireland ambaye alimpachika mimba dada yake na kuzaa naye mtoto kabla ya kugundua kuwa ni ndugu yake, anafunga ndoa na dada yake huyo mwishoni mwa mwezi huu.
James na Maura, ambao ni kaka na dada ambao wamezaa mtoto mmoja, wanategemea kuvalishana pingu za maisha mwishoni mwa mwezi huu.

Ndugu hao ambao wameamua kubadilisha majina yao halisi ili wasijulikane na jamii, waliangukia kwenye penzi zito bila ya kutambua kuwa wamezaliwa kutokana na baba mmoja.

"Itakuwa ni harusi ndogo, tuna mashahidi wawili tu ambao tunawafahamu vizuri na wanaelewa hali tuliyo nayo", alisema James

"Hatujui kama baba yetu atakuja kwenye harusi au kama mama zetu watahudhuria harusi yetu".

"Mtoto wetu wa kiume anasubiria kwa hamu harusi yetu na anaelewa kinachoendelea, hatujali kuoana mtu na dada yake", aliongeza James.

James na Maura walizaliwa kutokana na baba mmoja na walikuwa wakiishi miji miwili tofauti iliyo mbali kwa kilomita 160.

James na Maura ambao hivi sasa wana umri kati ya miaka 20-28, Walikutana miaka michache iliyopita kwenye ukumbi wa starehe katika mji mwingine wa tatu na kuangukia kwenye penzi zito na walipata mtoto wa kiume miaka miwili baadae.

Waligundua kuwa ni ndugu mwaka jana wakati wa krismasi wakati mama yake James alipomuambia James kuwa baba yake wa kweli siyo mwanaume aliyemlea miaka yote.

Mwezi wa nne mwaka huu walithibitisha kuwa ni mtu na dada yake baada ya vipimo vya DNA kuthibitisha kufanana kwa DNA zao.

James na Maura walielezea jinsi wanavyoisubiria kwa hamu harusi yao pamoja na kwamba wanajua kuwa sheria za nchi haziwaruhusu kufunga ndoa.

Kutokana na kwamba kitambulisho cha James kinaonyesha jina la baba yake kuwa ni Vincent ambalo ni jina la mwanaume aliyemlea, kipingamizi cha kisheria cha kuzuia ndoa yao kinakuwa kimeepukika kwani majina ya baba kwenye vitambulisho vyao yatakuwa tofauti.


source nifahamishe